Waziri wa maji na umwagiliaji Mh.injinia Isack Kamwelwe ameoneekana kulidhishwa na ujenzi wa miradi ya maji katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga.Katika ziara yake ya kikazi ndani ya Mji wa Mafinga iliyokuwa na lengo la kukagua maendeleo ya miradi ya maji inayotekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga alitembelea ujenzi tanki la kuhifadhia maji lililojengwa eneo la kinyanambo lenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya lita laki tano ambazo zitatumiwa na wananchi wapatao 15000 ambao ni wanufaika wa mradi.
Waziri alisema '' lengo la serikali ni kutatua kero ya maji kwa asilimia 95 kwa wakazi wa mjini ifikapao 2020'' ambapo jumla ya fedha kiasi cha shilingi milioni mia nne na saba zilitolewa na wizara yake ya maji na umwagiliaji na kuwezesha ujenzi wa tanki hilo la kuhifadhiwa maji kujengwa katika eneo la kinyanambo, aidha katika hatua nyingine wizara ya maji na umwagiliaji kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Mafinga imanza tena mchakato wa ujenzi wa tanki jingine kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi ujazo wa maji kiasi cha lita milioni moja katika eneo la changarawe na tenda tayari imeshatangazwa toka tarehe 15/12/2017, tanki hilo ambalo litagharimu jumla ya bilioni moja.
Lengo la Halmashauri ya Mji wa Mafinga ni kuhakikisha rasilimali za maji zinapatikana na kuendelezwa kwa manufaa ya wananchi kwa kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana kwa umbali usiozidi mita mia nne kwa mujibu wa sera ya maji ya 2002, mpaka sasa asilimia 69 ya wakazi wa Mji wa Mafinga wanapata maji safi na salama
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.