KAULI MBIU
"AJENDA 10/30: KILIMO NI BIASHARA, SHIRIKI KUHESABIWA KWA MIPANGO BORA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI'
Halmashauri ya Mji Mafinga ni moja kati ya Halmashauri zitakazo Shiriki maonesho ya wakulima nanenane yatakayo fanyika kitaifa Jijini Mbeya.
Sekta mbalimbali zitashiriki maonesho haya yatakayoanza tarehe 1/8 na kufikia kilele chake tarehe 8/8.
Michakato mbalimbali ya kutafuta wakulima na wafugaji bora kwa Halmashauri ya Mji Mafinga imetekelezwa,
Aidha katika Banda la Halmashauri ya Mji Mafinga sekta mbalimbali zitashiriki ambapo vitu vifuatavyo vitaonyeshwa:-
Kilimo Bora cha Parachichi, Mahindi, Alizeti na Mbogamboga.
Ufugaji bora wa ng'ombe wa Maziwa, Kuku, Samaki na Sungura
Uongezaji thamani wa mazao ya kilimo na mifugo
Mazao ya Misitu- Miche ya Miti, Mbao na Asali
Uongezaji thamani wa mazao ya Misitu na Nyuki
Lishe
Shughuli za Utalii pamoja na Fursa za uwekezaji.
Hakikisha ukiwa Jijini Mbeya unatembelea banda letu Halmashauri ya Mji Mafinga.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.