“Wajibu wa kutoa huduma na kumsikiliza mwananchi ni wajibu wa mtumishi wa umma kutokuwa na hasira na kutoa huduma kwa weledi kwa Wananchi” Akizungumza Charles Mwaitege katika mafunzo ya Ajira Mpya amewataka Watumishi wapya kufuata miongozo ambayo wamefundishwa kuhusu Utumishi wa Umma kwani kwa kufanya ivyo wataweza kuwahudumia Wananchi vizuri na kutoa huduma bora kwa jamii.
Pamoja na hayo amewataka pia kuwa na heshima mahali pa kazi na kuheshimiana bila kujali umri wa mtu kwani kwa kufanya hayo amesema watatengeneza umoja na kufanya kazi kwa ushirikiano ambao utaleta tija kwa Nchi yetu kwa ujumla pia amesisitiza kwa Watumishi wapya kutoa huduma kwa wakati na bila kubagua Mwananchi yoyote kwani watu wote wanastahili huduma bora.
Pia Wataalamu wa Tehama wamewafundisha Watumishi wa Ajira Mpya kuhusu Mifumo mbalimbali ya Kiutumishi na Kiutendaji ikiwemo MUKI ambao ni mfumo wa kujifunza kieletronic kwa Watumishi wa ajira Mpya.
Mafunzo haya ni mwendelezo wa utaratibu uliowekwa na Halmashauri ya Mji Mafinga wa kutoa uelewa kuhusu miongozo na masuala ya Kiutumishi kwa Ajira Mpya.
Na yameudhuliwa na Watumishi ambao ni ajira Mpya kutoka idara mbalimbali pamoja na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Mji Mafinga ambao walikuwa wakitoa mafunzo.
Na,
Anna Mdehwa,
Afisa Habari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.