Akiwasilisha rasimu ya Mpango wa Bajeti ya 2025/2026 kwa Baraza la Waheshimiwa Madiwani Afisa Mipango Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Peter Ngussa kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella amesema kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri ya Mji wa Mafinga inakadiria kutumia Jumla ya Tsh. 31,558,031,000.00 kati ya fedha hizo Tsh. 7,638,590,000.00 zitatokana na mapato ya ndani, Tsh.942,454,000.00 ni ruzuku ya matumizi mengineyo (OC), Tsh. 17,395,844,000.00ni ruzuku ya mishahara na TZS 5,581,143,000 ni ruzuku ya Miradi ya Maendeleo.
JUMLA KUU BAJETI YA MWAKA 2025/26 31,558,031,000.00
Ngusa amesema Halmashauri ya Mji Mafinga katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 imejiwekea vipaumbele vinne ambavyo ni:-
-Kutekeleza miradi inayolenga kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani (Own Source), mathalani:
Kununua maeneo ya uwekezaji,
Kuendeleza ujenzi wa miradi ya kimkakati,
Kuendeleza shamba la parachichi Makalala,
Kutunga na/au kuhuisha sheria ndogondogo za ukusanyaji wa mapato.
-Kuboresha utoaji wa huduma za jamii kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii kwa ukamilisha/kujenga miundombinu ya Sekta
-Kuboresha ustawi wa wananchi kwa kuimarisha utawala bora kwa kuzingatia: demokrasia, utawala wa Sheria, haki, ushirikishwaji wa wananchi.
-Kuimarisha Hali ya usafi na Uhifadhi wa Mazingira katika Mji wa Mafinga.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amewapongeza Wataalamu chini ya Mkurugenzi Mji Bi.Fidelica Myovella amesema kwa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na Ukusanyaji wa Mapato ambapo mwaka jana makusanyo yalikuwa 6.6 ambapo kwa mwaka 2025/2026 makusanyo yameongezeka mpaka kufikia Bilioni 7.6.
Baraza la Bajeti limehudhuriwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi Ndugu Reuben Chongolo na Wataalamu kutoka Tarura na Mauwasa.
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.