“Jumla ya Wanafunzi 68 wanahitimu leo ikiwa Wavulana 27 na Wasichana 41, Wahitimu hawa ni ushahidi wa kazi nzuri iliyofanywa na Walimu,Wazazi na Uongozi wa Shule kwa pamoja ambapo tumeweza kufikia hapa na pia nawaomba Wazazi mwendelee kuonyesha ushirikiano katika masomo ya watoto wenu kwani ndo kwanza hatua ya awali katika safari ya Elimu ya Watoto wetu”. Kauli hii imetolewa na James Kelela Mkuu wa Shule ya Chief Mkwawa. Katika Mahafali ya Chekechea yaliyofanyika katika ukumbi wa shule hiyo.

Aidha amewashukuru Wazazi kwa kuendelea kuwaamini na kuwapeleka Watoto wao shuleni hapo na amehaidi kuendelea kuboresha Mazingira bora ya Shule na miundombinu ikiwa kuanzisha mafunzo ya Tehama kwa Wanafunzi ngazi ya awali na Msingi.

Chief Mkwawa English Medium Primary School ni moja ya shule ya Msingi yenye mchepuo wa kiingereza inayomilikiwa na Halmashauri ya Mji Mafinga ambapo ilianza mwezi wa kwanza 2024. Na mpaka kufikia sasa inajumla ya Wanafunzi 365, Wavulana 183 na Wasichana ni 182 na Walimu 13 ikiwa na darasa la juu zaidi ni Darasa la Tatu.
Na,
Anna Mdehwa,
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.