“ Watumishi hakikisheni hamuwafokei wananchi wala kuwafanya waichukie Serikali kwaajili ya huduma Mbaya tunazotoa, Msiwabague wananchi toeni huduna kwa haki, upendo na unyenyekevu na kwa kufuata maadili ya utumishi wa Umma bila kuomba wala kutaka rushwa kwani sisi watumishi ni taswira ya Serikali “

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Mufindi Ndugu, Abdull Abdarahmani alipokuwa akizungumza na watumishi wa Ajira Mpya zaidi ya 102 wa Halmashauri ya Mji Mafinga kwenye Semina Elekezi kwa waajiriwa wapya kutoka Idara mbalimbali zikiwamo sekta za Utawala, Afya, Elimu Msingi na Sekondari ,Maliasili, Mazingira, Ukaguzi na Habari.

Abdull amesema kuwa Wananchi wakitendewa vibaya katika kuwapa huduma wanapeleka chuki yao kwa Serikali iliyopo madarakani, wakati huduma mbovu imetolewa na mtumishi mmoja ambaye ameshindwa kufuata misingi na maadili ya kazi yake, hivyo amewataka watumishi kuhakikisha wanailinda Taswira nzuri ya Serikali kufuata miongozo ya kazi na kuwa wabunifu katika kazi zao ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kama ambavyo Serikali imeweka Malengo.
Akifungua Semina Hiyo Elekezi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mkurugenzi Bi. Fidelica Myovella amewataka watumishi hao wa Ajira Mpya kuwa vinara katika kazi na moyo wa utendaji kazi waliokuja nao usififishwe na watumishi wachache wanaotaka kuzima ndoto zao huku wakijiepusha na utoro na Ulevi kazini”

“ Tunaishukuru Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta watumishi katika Halmashauri yetu na kuboresha miundombinu ya sekta mbalimbali ikiwamo za Elimu na Afya. Hakika kwa kupata watumishi hawa tunauhakikika wananchi wataendelea kupata huduma kwa wakati”
Semina hiyo Elekezi imehudhuriwa pia na Mkuu wa Idara ya rasilimali watu Ndugu Charles Mwaitege, Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Bi Doroth Kolelo na wakuu wa Idara mbalimbali zikiwamo Taasisi za Benki na Mifuko ya jamii, ambapo mafunzo ya awali yaliyotolewa.
Imeandaliwa na
Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mji Mafinga
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.