Halmashauri ya Mji Mafinga imeanza kutambua na kuweka mikakati ya kutokomeza Udumavu kwa kuwapa motisha Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii wanaofanyakazi kwa kutumia juhudi binafsi kupambana na udumavu na Utapiamlo.
Akizungumza wakati wa kutoa zawadi na vyeti kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii Dkt. Linda Salekwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi amesema Elimu kubwa ya uhamasishaji kwa wajasiliamali wadogo wadogo na Wafanya biashara inatakiwa kuhusu umuhimu wa Lishe na kupambana na utapiamlo kwa watoto chini ya miaka 2.

“ Nashauri Kama Halmashauri tuje na Mkakati wa utoaji wa Elimu kwa wajasiliamali wadogo Kwani imebainika kuwa baadhi ya watoto chini ya umri wa miaka 2 ambao wanashinda na wazazi kwenye shughuli zao au majumbani wamegundulika kuwa na utapiamlo kulingana na takwimu.”

“Tuna kazi ya ziada ya kufanya kupunguza tatizo la Lishe. Tuhakikishe tunalimaliza kabisa tatizo la utapiamlo. Tuhakikishe Mzazi anapoenda kliniki anapewa elimu ya Lishe, Tusifanye mambo yale yale yasiyoleta mabadiliko, tuje na mipango na mikakati mipya kama ambavyo Leo tumeweza kuwatambua wahudumu wa Afya wanaofanya vizuri kwa kipindi cha robo ya kwanza ya 2025/2026, “Amesema Dkt. Linda Salekwa
Mmoja wa Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii aliyepata cheti na zawadi kwa kuhamasisha wakina mama kuhudhuria Klinik siku ya lishe Bi Cecilia Myinga kutoka Kata ya Bumilayinga amesema zawadi hii imempa hari na chachu ya kufanya kazi kwa bidii zaidi Kwani hata Serikali imetambua mchango wake.

Kikao hicho cha Tathmini ya Hali ya Lishe kwa robo ya kwanza 2025/2026 kimehudhuriwa pia na Mkurugenzi MJI Mafinga Bi. Fidelica Myovella, WAKUU wa IDARA na Watendaji wa Kata zote za Halmashauri ya MJI Mafinga.
Na Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.