Kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi na shughuli za kibinadamu za uvunaji wa mazao ya misitu na kilimo kisichofuata hifadhi ya mazingira na vyanzo vya maji halmashauri ya mji wa mafinga imejiwekea lengo kwa mwaka 2020 kuotesha miche 1,500,000 ambapo hadi sasa tayari jumla ya miche 448,350 imeshapandwa katika maeneo mbalimbali ya halmashauri,akisoma taarifa ya halmashauri katika uzinduzi huo mbele ya mgeni rasmi ndugu Joseph mchina ambae alimuwakilisha mkuu wa wilaya ya mufindi afisa mazingira wa halmashauri bwana Tuyi alisema ‘’halmashauri ya mji wa mafinga imeandaa jumla ya miche 1000 aina ya miti maji ambayo itapandwa katika zoezi hili na miche 350 itasambazwa kwenye taasisi za shule na vituo vya afya na miche 750 itapandwa eneo la kando kando ya barabara ya tanzam lakini pia halmashauri imeanzisha kitalu cha miche 13,530 imepandwa ambayo itapandwa katka maeneo mbalimbali ya mji’’ alisema Tuyi.
Halmashauri ya mji wa mafinga ni moja kati ya halmashauri nchini zinazoongoza katika upandaji miti na utunzaji wa mazingira kwani kwa mwaka 2019/2020 halmashauri imekuwa mshindi wa tatu kitaifa katika halmashauri zinazoongoza katika utunzaji wa mazingira.Ikumbukwe kuwa serikali iliamua kutenga siku maalum ya upandaji miti kitaifa kufuatia mabadiliko ya tabianchi
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.