Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro alifika eneo la Changarawe Mjini Mafinga ilipotokea ajali iliyopoteza maisha ya watu 20 na kusababisha majeruhi 7.
IGP Simon Sirro ametoa maagizo kwa jeshi la Polisi Mkoani Iringa kitengo cha Usalama Barabarani kuhakikisha wanafanya ukaguzi kwa madereva wanaosafirisha abiria.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Saada Mtabule amelipongeza jeshi la polisi nchini kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Viongozi mbalimbali wa Wilaya waliambatana na Mkuu wa Wilaya kupokea ugeni huo.
Imeandaliwa na Ofisi ya Habari na Mawasiliano -Mafinga Mji.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.