Na: Sima Bingileki
Leo tarehe 14/6/2025 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Lugalo Timu ya wasichana wenye mahitaji Maalumu kutoka Iringa imetikisa nyavu za Wasichana Kagera kwa goli 13-1 kwa vipindi viwili.
Akizungumza Mratibu wa wa Mchezo wa Goli (Goal ball) Anitha Mlay amesema Mchezo huu unazidi kukua kwa kasi kwani kila mwaka Timu zinaongezeka na mwaka huu 2025 jumla ya mikoa 24 inashiriki Mchezo huu na Mikoa imejipanga vizuri katika kushiriki na kutimiza mahitaji ya watoto hawa wenye mahitaji maalum.
“ Hakika tunaishukuru sana Serikali kwa kuona umuhimu wa mchezo huu wa Goal Ball na kuwapa umuhimu wanafunzi wenye mahitaji maalumu kipaumbeke kwani ushiriki umekuwa mkubwa na hakuna changamoto ambayo watoto wanakutana nayo katika kucheza mchezo huu, mwaka jana ushiriki katika mchezo huu ulikuwa mikoa 22 mwaka huu mikoa imeongezeka na kuwa 24 hivyo hamasa imekuwa kubwa na jamii imeelewa umuhimu wa mchezo huu” Amesema Anitha Mlay
Amesema leo tarehe 14/6/2025 jumla ya mechi 9 zimechezwa katika hatua za Makundi ambapo Shinyanga imeipiga Rukwa 12-6(me)
Ruvuma imeipiga Arusha 9-2(me)
Njombe imeipiga Mbeya 21-2(me)
Dar-es salaam imeipiga Tanga 8-3( me)
Katavi imeipiga Morogoro 12-2(me)
Pwani imeipiga Rukwa 7 -5(me)
Kagera imeipiga Tabora 12-3( me)
Pwani imeipiga Kilimanjaro 6-5( me)
Iringa imeipiga Kagera 13-2( ke)
Mashindano ya mwaka 2024 Mkoani Tabora, timu za mpira wa Goal Ball Morogoro wavulana, na Njombe wasichana ziliibuka kuwa Mabingwa .
Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA yanaandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Utamaduni na Michezo ambapo yanaongozwa na Kauli mbiu “Viongozi bora ni msingi wa maendeleo na Taaluma, Sanaa na Michezo,Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu”
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.