JUMLA YA VIWANJA 1305 VIMEPIMWA KATIKA MPANGO WA MKURABITA NA HATI MILIKI 680 ZIMELIPIWA ADA YA UMILIKISHWAJI- DC MUFINDI AKABIDHI HATI KWA WANANCHI KATA YA UPENDO-MKURABITA.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Saad Mtamule amekabidhi Hati miliki za Ardhi kwa wananchi wa Kata ya Upendo Mtaa wa Lumwago katika mpango wa MKURABITA ambapo jumla ya viwanja 1305 vimepimwa na Hati 680 tayari zimelipiwa na wananchi kwaajili ya umiliki.
Akizungumza wakati wa utoaji hati hizo kwa wananchi Mheshimiwa Mtambule amesema Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan inajali sana wananchi wake kwani imegharamia kupanga na kupima ardhi na wananchi wanalipia tu ada ya umiliki.
“Wananchi Hati zilizolipiwa ni 680 na Serikali imegharamia kupima na kupanga hivyo naomba niwasisitize wale ambao hamjalipia Ada za Hati zenu mfanye hivyo mapema kwani lengo la Serikali ni kuleta Maendeleo kwa wananchi wake kwa kupunguza umaskini na kuinua hali za Uchumi.
Naye Mtendaji Mkuu wa MJpango wa MKURABITA CPA DK. Seraphia Mgembe amesema lengo la Mpango ni kuhakikisha wananchi wanamiliki Uchumi wao kwa kuwa na Hati ambazo zitasaidia kuondoa migogoro ya Ardhi na kukuza uchumi wa wananchi wanyonge.
Akitoa taarifa ya MKURABITA Afisa Mipango Miji Ndugu, Rajab Bogwa amesema lengo la Mpango ni kupima viwanja 1000 lakini muitikio umekuwa ni mkubwa hivyo viwanja 1305 vimepimwa tayari na wananchi wamechangia gharama za Umiliki ambapo Serikali imetumia takribani shilingi Milioni 75 katika Kuandaa kupima ardhi.
Zoezi limehudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashari ya Mji wa Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge, Waheshimiwa madiwani viti maalumu, Diwani wa kata ya Upendo Mheshimiwa Michael Msite, Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi Happiness Laizer, wataalamu ngazi ya mkoa wananchi na waandishi wa habari
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO-MAFINGATC
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.