Jumlaya Watahiniwa 3499 wavulana 1762 na Wasichana 1737 Wanatarajia kufanya Mtihaniwa Upimaji wa Kitaifa kwa Darasala Nne 2024 katika Halmashauri Ya Mji Mafinga.
AkizungumzaMkurugenzi wa Halmashauri ya Mji MafingaBi. Fidelica Myovella amesema Mtihaniutafanyika siku mbili kuanzia Tarehe 23 hadi Tarehe 24 Mwezi Oktoba na Idadi yaShule zitakazo fanya Mtihani ni shule 45, Shule za Serikali 31 na Shule Binafsi14.
BiMyovella ametembelea baadhi ya Shule zitakazofanya Mtihani wa Upimaji waDarasa la Nne katika Halmashauri ya Mji Mafinga kwenye Shule ya msingiMamba iliyopo kata ya Isalavanu yenye Watahiniwa 86 na Shule ya Msingi Kilimaniyenye watahiniwa 46
Bi.Myovella amepata fursa ya kuzungumza na wanafunzi na kuwatakia kila lakherikatika Mitihani yao.
NaeAfisa Elimu Msingi Mwalimu Dorothy Kobelo amesema maandalizi yote yamekamilikakwa ngazi ya Halmashauri na Shuleni maandalizi yamekamilika hivyo amewatakaWalimu kutoa ushirikiano wa kutosha kwa zoezi hilo la Kitaifa.
AidhaBi Myovella amewataka wazazi wa wanafunzi wanao tarajiwa kufanya Mtihani waTaifa kuwa Bega kwa bega na watoto wao vile vile kuepuka kuwapa msongo wamawazo ambao utawakosesha wanafunzi utulivu wa kufanya Mitihani.
Imeandaliwana Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
SimaBingileki
Afisa HabariMkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.