KUELEKEA MIAKA 61 YA UHURU-MAFINGA TC WATEMBELEA WAGONJWA
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Saad Mtambule akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Happiness Laizer akiongoza Watumishi wa Mji, wameshiriki kufanya Usafi wa Mazingira katika maeneo yote yanayozunguka Hospitali ya Mji Mafinga na kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika Hospitali hiyo.
Akizungumza na watumishi wa Taasisi mbalimbali walioshiriki zoezi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Saad Mtambule amesema kuwa Waasisi wetu walipambana mpaka kuhakikisha nchi yetu inapata uhuru hivyo, ili kuonyesha mchango wetu kwa nchi yetu basi na sisi tufanye kazi kwa bidii bila kuchoka kuhakikisha katika sekta zote Maendeleo chanya yanapatikana ili wale waliochini yetu wanaotutegemea waweze kufaidi matunda ya nchi yao.
“ Tuhakikishe tunafanya kazi kwa bidii tusimamie miradi ya maendeleo na tutoe huduma Bora kwa wananchi ili waisemee vizuri Serikali kwa yale maendeleo yaliyopatikana baada ya uhuru”
Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada katika wodi ya wanawake katika Hospitali ya Mji Mafinga Mkurugenzi Bi Happiness Laizer amesema lengo la Serikali Ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma Bora na kwa wakati hivyo kuwatembelea wagonjwa Ni kuonyesha upendo, kuwajali na kuwathibitishia kuwa Serikali ipo pamoja nao kwa nyakati zote.
Serikalini imeendelea kuboresha huduma za Afya kwa kujenga miundombinu Bora ili kuhakikisha wananchi wanapokea huduma na kwa gharama nafuu.Taasisi mbalimbali zimehudhuria zoezi Hilo la kuelekea miaka 61 ya Uhuru ikiwemo Saohill, Nssf,Taasisi za kifedha pamoja na watumishi wa hospitali ya Mji Mafinga.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru ni “ Amani na Umoja Ni Nguzo ya Maendeleo Yetu”
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga Tc
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.