KUFANYIKA KWA MTIHANI WA TAIFA WA KUMALIZA KIDATO CHA NNE TAREHE 17/11/2025 HADI TAREHE 5/12/2025
Posted on: November 17th, 2025
Jumla ya Watahiniwa 2,176 wanatarajiwa kufanya Mtihani wa kumaliza Kidato cha nne, katika Halmashauri ya Mji Mafinga ikiwa wavulana ni 1,102 na Wasichana ni 1,074, kati ya hao watahiniwa walioko katika mfumo rasmi ni 2,069 ambapo wavulana ni 1,037 na Wasichana 1,032. Watahiniwa wa kujitegemea jumla yao ni 65 ikiwa Wavulana ni 42 na Wasichana ni 107.
Akizungumza Mkurugenzi wa Halmashauri ya MJI Mafinga Bi. Fidelica Myovella amesema Mtihani huo wa Taifa wa kumaliza kidato cha Nne utaanza tarehe 17/11/2025 mpaka tarehe 5/12/2025 ambapo Shule za Binafsi ni 11 na Shule za zinazomilikiwa na Serikali ni 11.
Aidha Katika Halmashauri ya Mji Mafinga Jumla ya Watahiniwa Jumla ya Watahiniwa 2,176 wanatarajiwa kufanya Mtihani wa kumaliza Kidato cha nne kutoka katika Shule za Sekondari 22 zikiwamo Shule 11 zinazomilikiwa na Watu Binafsi na Shule 11 Zinazomilikiwa na Serikali .
Myovella anawaomba wazazi na walezi kuwapa ushirikiano watahiniwa na Mazingira mazuri ya kufanya Mtihani ili waweze kuwa na utulivu na kufaulu.
Imetolewa na
SIMA MARK BINGILEKI
MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
17/11/2025