“Maafisa Habari Hakikisheni wananchi wanapata taarifa sahihi na mnatangaza Miradi ya Maendeleo inayofanywa na Serikali”
“Hakikisheni mnatumia taaluma yenu, kuandika kupinga rushwa, kuhakikisha wanawake vijana na watu wenye Ulemavu wanapata fursa sawa na kupata haki ya kupata taarifa”
Kauli hiyo imetolewa na Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdul Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar alipokuwa akifungua kikao cha 20 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kilichofanyika katika Ukumbi wa Aman Zanzibar.
Amesema kikao hiki cha 20 cha Maafisa Habari kitasaidia wataalamu hao Kujadiliana, kubadirishana uzoefu kwa lengo la kujadili mbinu na kutafuta namna ya kuitangaza Serikali ili wananchi wajue nini Serikali inafanya.
Nae Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Prof. Palamagamba Kabudi amesema Kikao hiki kinawakutanisha maafisa habari ambao ni muhimu kwa ustawi wa Taifa la Tanzania na ni mala ya kwanza kufanyika Zanzibar.
“Muwe Mabalozi wazuri wa kuitangaza Zanzibar
Kuitumia vizuri fursa hii kujadiliana na kubadilishana uzoefu ili mkitoka hapa mkatangaze kwa usahihi kazi zilizofanywa na Serikali na wananchi wajue nini Serikali imefanya .
Kikao hicho kimehudhuriwa Viongozi wakuu wa Serikali, Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali kutoka Tanzania Bara na Visiwani na Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka Mkoa wa Iringa. Jumla ya Maagizo 7 yalitolewa.
Imeandaliwa na Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.