Halmashauri ya Mji Mafinga yavuka lengo la ukusanyaji Mapato ya Ndani kwa mwaka wa fedha 2023/2024 yakusanya Bilioni 6.2 ikiwa ni sawa na asilimia 113 kutoka Bajenti pangwa ya shilingi Bilioni 5.52
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika leo tarehe 14/8/2024 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Luganga.
Akifungua Mkutano huo wa Baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za robo ya nne kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 Mwenyekiti wa Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amesema matokeo hayo yametokana na Ushirikiano baina ya Mkurugenzi na Timu yake na Waheshimiwa Madiwani kushauriana na kuwa kitu kimoja linapofika suala linalogusa maslahi mapana ya Halmashauri
“Mapato ndio uhai wa Halmashauri yoyote , hakika niwapongeze kwa kuvuka lengo na kukusanya asilimia 113. Hii iwe chachu ya kujituma zaidi. Mafinga imekuwa ikifanya vizuri katika usimamizi wa Miradi ya Maendeleo na imekuwa ikifanya vizuri kwenye sekta mbalimbali, hii inatupa nguvu sisi viongozi kuzidi kufanya kazi na kuwatumikia wananchi kwa Uadilifu Mkubwa” Dkt. Linda Salekwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi
Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mufindi Ndugu Clemence Immanuel Bakuli amesema Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi unaonekana kwa vitendo katika Halmashauri ya Mji Mafinga. Amesema huduma zinatolewa kwenye sekta za Afya,Elimu. ukusanyaji wa Mapato na zaidi Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo hauna mashaka.
Mkutano wa Baraza la Waheshimiwa Mqdiwani umehudhuriwa na Wananchi, Mwakilishi ngazi ya Mkoa,Kaimu Katibu Tawala Wilaya , Wakuu wa Idara na Vitengo na Waandishi wa Habari.
Imeandaliwa na
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.