Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella amefanya Kikao kazi na Watumishi wa Ajira Mpya katika Ukumbi uliopo katika Ofisi za Halmashauri na kuwasisitiza kuzingatia Uwajibikaji katika Utendaji wa Majukumu Yao.
Akizungumza katika kikao hicho Bi, Fidelica Myovella amesema Watumishi wa Ajira Mpya Wanatakiwa kumshukuru Mungu na Serikali kwa kuwapatia Ajira hivyo Wanatakiwa kufanya kazi kwa Weledi kwa kutoa Huduma nzuri kwa Jamii,pia Wazingatie Maadili ya Kazi kwa kuvaa Vizuri,kutumia Lugha nzuri ya Mawasiliano na Kuboresha Ushirikiano katika Maeneo ya Kazi.

Naye Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Mufindi Ndugu Abdull Abdarahaman amewasihi Watumishi wa Ajira Mpya kutunza vyema Vifaa vya huduma za Umma na kutanguliza maslahi ya Umma mbele kuliko maslahi binafsi pia huduma zitolewe kwa Wakati na unyenyekevu bila kujali rangi au kabila ya Mtu.
“Mnapokuwa Maeneo ya Kazi tumieni Lugha nzuri na zingatieni suala la Mavazi ya heshima na muepuke kutoa au kupokea rushwa pia muwe na Utii na Serikali iliyopo Madarakani kwa kutekeleza Sera,Kanuni na Miongozo inayotolewa na Viongozi wetu.” Amesema.

Pamoja na hayo Mkuu wa Idara ya Utumishi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Charles Mwaitege amewahimiza Watumishi wa Ajira Mpya Kutojihusisha na mambo ya Siasa,kuepuka ulevi na Mikopo isiyo ya lazima pia kuzingatia muda wa Kazi, kuonyesha Ushirikiano Wanapokuwa kazini na kutoshiriki kupinga Sera au Mipango ya Serikali.
Wakati huo huo Afisa Utumishi Ndugu Julius Mwalongo ametoa Mafunzo juu ya Upimaji wa Utendaji Kazi na kuwahimiza Watumishi wa Ajira mpya kuwa na Utaratibu wa kujaza majukumu kwenye mfumo.

Mkurugenzi Bi, Fidelica Myovella ameendelea kumshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwasaidia kuwaongezea Watumishi wa Ajira Mpya ambao watasaidia katika Utekelezaji wa Majukumu katika Idara na Vitengo vya Halmashauri ya Mji wa Mafinga.
Vedasto Faustine Malima
Afisa Habari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.