“Niwapongeze kwa mchango mkubwa mnaotoa katika jamii hasa katika kudumisha maadili na kuwa mstari wa mbele kukemea maovu na kutoa ushauri unaosaidia kuimarisha malezi, amani na utulivu kwa jamii.” Kauli hii imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovela wakati wa ziara ya kikazi ya Baraza la Wazee la Mkoa lilipotembelea Baraza la Wazee la Halmashauri ya Mji Mafinga.

Katika ziara hiyo, Bi. Myovela pia amekabidhi nakala za Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 (Toleo la 2024) kwa Wajumbe wa Baraza hilo, ili kuwapatia uelewa mpana kuhusu haki na wajibu wa Wazee nchini.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Halmashauri ya Mji Mafinga, Ndugu Daniel Mwaisela, ameishukuru Serikali kupitia Halmashauri ya Mji Mafinga kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakipewa kwa kuendelea kuwashirikisha katika shughuli mbalimbali za kijamii na kitaifa.

Bi. Myovela amesisitiza kuwa Halmashauri itaendelea kushirikiana kwa karibu na Mabaraza ya Wazee kuhakikisha kundi hilo muhimu linapata huduma bora na linashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Sera na Mipango ya Maendeleo.
Na,
Anna Mdehwa,
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.