Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Fedelica Myovella leo amekabidhi pikipiki mbili kwa Maafisa Maendeleo ya jamii katika Kata ya Isalavanu na Bumilayinga ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa wananchi kikamilifu.
Pia Bi Myovella amewataka Maafisa Maendeleo kuhakikisha wanatumia pikipiki hizo katika kufatilia vikundi ambavyo vimepewa mikopo ya uwezeshaji kiuchumi ili viweze kufanya marejesho kwa wakati na kutoa elimu kwa vikundi vyote.

Aidha aimeishukuru serikali kwa kutoa pikipiki hizo ili kurahisisha huduma kwa wananchi na pia ametoa rai kwa Maafisa hao kuhakikisha wanavitunza vyombo hivyo kwa umakini mkubwa na kuacha kuvitumia kama bodaboda .
Michael Ngowi Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.