“ Mkikagua kazi Mkajiridhisha kwa kushirikiana na Mhandisi muwalipe mafundi wasicheleweshwe malipo yao,ila msilipe kabla ya kujiridhisha na kukagua kazi zinazoendelea za Ujenzi katika maeneo yenu”
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella alipokuwa akifanya ziara ya ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika ngazi ya Kata.
Akiwa ameigozana na Afisa Mipango Bwana Peter Ngusa na Afisa Utumishi Ndugu Charles Mwaitege Mkurugenzi ametembelea Ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Sekondari Isalavanu, Shule ya Sekondari Nyamalala ujenzi wa madarasa 2 na Maabara 2, ujenzi wa nyumba za watumishi zahanati ya Saohill na Ujenzi wa madarasa mawili na na ukamilishaji wa bwalo la chakula katika Shule ya Mchepuo wa kingereza( English Medium) Chief Mkwawa
Aidha kupitia Mapato ya ndani Halmashauri inajenga jengo la Mama Na Mtoto na Chumba cha Upasuaji katika Zahanati ya Upendo ambapo mpaka kukamilika kwake jengo litagharimu kiasi cha shilingi Milioni 250, Mpaka sasa Halmashauri imetumia jumla ya shilingi milioni 170 kwa hatua iliyofikia.
Ni utaratibu wa kawaida kwa Timu ya Menejimenti kufanya ziara ya Ufuatiliaji kwenye miradi ya maendeleo lengo likiwa kuhakikisha Hakuna changamoto yoyote katika ukamilishaji wa miradi hiyo na kuhakikisha ubora wa miradi katika hatua za awali za ujenzi.
Kupitia mapato yake ya ndani Halmashauri inajenga miradi mikubwa ambayo ni Shule inayomilikiwa na Halmashauri ya Mchepuo wa Kingereza( English Medium) Chief Mkwawa na Jengo kubwa la Mama na Mtoto na chumba cha upasuaji katika zahanati ya Upendo.
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.