“ Muitikio ni Mkubwa kwa wananchi wa Mafinga Mji, tunachojitahidi kufanya ni kuhakikisha kila mwananchi anayejitokeza kwaajili ya Uandikishaji wa Daftari ka Kupigia kura anapata haki yake ya kuandikishwa na kuboresha taarifa zake, kwa kuongeza mashine za BVR sehemu ambazo kuna wananchi wengi.”
Akizungumza wakati wa kukagua zoezi la Kuandikisha Wapiga Kura Halmashauri ya Mji Mafinga yenye vituo 78 Afisa kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Hezron Tungaraza amesema vituo 8 vilivyokaguliwa leo tarehe 30 Disemba 2024 muitikio wa wananchi hasa maeneo ya Mjini umekuwa Mkubwa mpaka kulazimu Kuongeza Mashine nyingine kwenye baadhi ya vituo ili kuhakikisha hakuna mwananchi anayebaki bila kuandikishwa
Aidha katika zoezi hilo la kukagua vituo Elimu ya Mpiga Kura imekuwa ikitolewa na Afisa Uwandikishaji Jimbo la Mafinga Mjini Ndugu Charles Mwaitege na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga sehemu zote ambazo kuna muitikio mkubwa wa wananchi ili kuwahimiza kuwaambia na wengine kuja kujiandikisha kabla ya zoezi kuisha.
Maeneo yaliyotembelewa ya kukagua zoezi la Uandikishaji ni Mtaa wa Balali, Gangilonga, Ifingo, JJ Mungai, Igawa, Ivambinungu.
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu Mafinga TC
Wataalamu kutoka Tume Huru yaTaifa ya Uchaguzi wakifatilia zoezi la uwandikishaji na uboreshaji wa taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura Jimbo la Mafinga Mjini.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.