Tarehe 26/9/2024 Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella ametoa Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwa Wadau katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Luganga.
Maelekezo hayo yanafafanua hatua zitakazoongoza Mchakato wa Uchaguzi, Kuanzia Uandikishaji wa Wapiga Kura, Uchukuaji na Urejeshaji wa Fomu za Kugombea, Uteuzi wa Wagombea na tarehe ya siku ya Uchaguzi.
Akitoa Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Wadau ambao ni Wazee maarufu, Viongozi wa Dini, viongozi wa Kisiasa, watendaji wa Kata. viongozi wa makundi maalumu Kama wanawake, bodaboda, Vijana na vikundi vya Uhamasishaji kutoka Halmashauri ya Mji Mafinga.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella Amesema :-
-Uchaguzi Utafanyika Tarehe 27 /11/2024
-Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura litafanyika kuanzia tarehe 11-20/10/2024 na vituo vitafunguliwa saa2:00Asubuhi na Kufungwa saa 12:00 Jioni.
-Kura zitapigwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi Mpaka saa 10:00 Jioni
- Wakazi wote wenye umri wa Miaka 18 au Zaidi wanahimizwa kushiriki uchaguzi
- Wakazi wenye Umri wa Miaka 21 au zaidi wanaotaka kugombea nafasi za Uenyekiti wa Mtaa/ Uenyekiti wa Kijiji/ Wajumbe wanahimizwa kuchukua fomu za kugombea katika Ofisi ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi
- Fomu zitatolewa na kutakiwa kurudishwa kuanzia tarehe1-7 Nobemba 2024
- Uteuzi wa wagombea Tarehe 8 Novemba 2024
- Pingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea tarehe 8-9 Novemba 2024 na Uamuzi wa Pingamizi tarehe 8-10 Novemba 2024
- Rufaa zitapokelewa kuanzia tarehe 10-13 Novemba 2024 na Uamuzi wa Kamati ya Rufaa utatolewa kuanzia tarehe 10-13 Novemba 2024
- Kampeni za Uchaguzi kwa Mujibu wa Kanuni Zitaanza Tarehe 20-26 Novemba 2024 kuanzia saa 2:00 Asubuhi hadi saa 12:00 Jioni.
Mgeni Rasmi katika kikao hicho cha kupokea Maelezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa ambaye amehimiza Amani na Uzalendo katika kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.