Natoa wiki moja kuanzia tarehe 13 Januari 2025 Wazazi na walezi hakikisheni wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na masomo katika Wilaya ya Mufindi wanaenda Shuleni, tarehe 20Januari, siku ya jumatatu tutafanya msako nyumba kwa nyumba, lengo ni kuhakikisha Ndoto za Mheshimiwa Rais zinatimia za wanafunzi kusoma bure na kupata elimu bora ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu bora ya Madarasa na vifaa”
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa alipokuwa akikagua mahudhurio ya siku ya kwanza ya wanafunzi ikiwa ni siku ya kwanza ya kufungua Shule kwa mwaka 2025.
Aidha amewataka walimu kuwapokea wanafunzi Shuleni hata kama hawana sare au michango yoyote lengo ni kupata elimu, hivyo sare isiwe kikwazo cha kuwazuia wanafunzi wasipokelewe Shuleni.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa amezungumza na wanafunzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Upendo ambayo imepangiwa wanafunzi 234 wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2025, pia ametembelea Shule ya Sekondari ya Amali Shule mpya ya Sekondari ambayo imepangiwa wanafunzi 36.
Kuhusu uandikishaji wa Awali Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa amezipongeza Halmashauri za Wilaya ya Mufindi Kwa kuendelea kuandikisha wanafunzi wa Awali ambapo kwa Halmashauri ya Mji Mafinga jumla ya wanafunzi 2109 wakiwemo wanafunzi 7 wa mahitaji Maalumu wameandikishwa.
Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mafinga TC
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt Linda Selekwa akiwa ametembelea shule mbalimbali kuangalia wanafunzi ambao wanaripoti kujiunga na kidato cha kwanza katika shule walizopangiwa.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.