Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Mufindi Bw Abdull Abdarahmani amewataka viongozi na watumishi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), wenyeviti wa bodi na viongozi wa Jumuiya za Watumia Maji ngazi ya Jamii kutoka wilaya za Mufindi, Kilolo na Iringa Mjini kuongeza uwajibikaji na kujiepusha na mgongano wa kimaslahi kwenye matumizi ya fedha katika utekekelezaji wa miradi ya maji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi ili thamani ya fedha ya miradi iweze kupatikana na kulinda hadhi na heshima ya Serikali.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba, 17,2025 na Abdarahmani wakati akiwasilisha mada ya Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma na Wajibu wa kila mtoa huduma katika kuzuia na kupambana na rushwa kwenye kikao cha robo mwaka kinachowakutanisha wadau wa maji kutoka mkoa wa Iringa, kilichofanyika ukumbi wa NFS, uliopo Halmashauri ya Mji Mafinga. chini ya uenyekiti wa Meneja wa RUWASA mkoa wa Iringa Mhandisi.
Mkuu huyo wa TAKUKURU wilaya ya Mufindi amewataka viongozi kutumia kikao hicho kufanya tathimini ya hali ya utoaji huduma ya maji ndani ya mkoa wa Iringa na kwamba wasione muhali kuwachukulia hatua watumishi na watoa huduma wachache wanaokwenda kinyume na Sheria, Kanuni na Miongozo.

Bwa. Abdarahmani aliwaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa maji hayana mbadala na kwamba Serikali inaendelea kuwekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji ili wananchi waweze kupata huduma bora, kinyume chake wananchi wanaweza kukosa imani kwa watumishi na Serikali yao hivyo watumishi hao wanapaswa kufanya kazi kwa weledi mkubwa.
Mkuu huyo wa TAKUKURU alizidi kueleza kuwa mgongano wa kimaslahi na usimamizi dhaifu wa matumizi ya fedha katika kutekeleza miradi ya maendeleo kunaweza kupelekea kuwa na miradi isiyo na ubora, kuwapata wakandarasi wasio na sifa/uwezo, miradi isiyokamilika kwa wakati na wakati mwingine kuna na huduma duni.
Aidha, Mkuu huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wadau kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 pasipo na kujihusisha na vitendo vya rushwa ili kupata viongozi wenye sifa na watakaosaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.