MKUU WA MKOA WA IRINGA MHESHIMIWA PETER SERUKAMBA AMALIZA MGOGORO WA WAFANYABIASHARA SOKO KUU LA MAFINGA ( VIBANDA 331)NA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA- WARIDHIA KUSAINI MIKATABA.
Akizungumza na Wafanyabiashara wa vibanda 331 wa Soko Kuu la Mafinga baada ya wafanyabiashara hao kuridhia kukaa na kufanya makubaliano badala ya tamko la awali la Mkuu wa Mkoa kuagiza Halmashauri ya Mji Mafinga kubomoa vibanda hivyo tarehe 22/5/2024.
Baada ya Mazungumzo ya Mkuu wa Mkoa na wafanyabiashara yafuatayo ni maridhiano:-
-KODI YA KILA KIBANDA ITAKUWA SHILINGI 80,000/- KILA MWEZI.
- MKATABA WA KIBANDA NI MIAKA 14 BAADA YA MUDA HUO KUISHA KIBANDA KITABAKI KUWA MALI YA HALMASHAURI.
-KATIKA MIAKA 14 YA MKATABA KIBANDA HAKITAKIWI KUUZWA KWA MTU YEYOTE.
- MADENI YA NYUMA YA KODI ZILIZOKUWA ZINADAIWA KABLA YA MGOGORO ZILIPWE NA WAFANYABIASHARA HAO KWA HALMASHAURI.
- MIKATABA YOTE KUFIKIA JUMATATU TAREHE 27/5/2024 IWE IMESAINIWA KUKIWA NA NAMBA YA NIDA NA JINA KAMILI LA MWENYE KIBANDA
-KODI ITALIPWA KILA MWEZI TAREHE 1-10 NA KAMA KODI HAIJALIPWA ITALIPWA NA FAINI YA ASILIMIA 5 YA KODI.
Mkuu Wa Mkoa wa Iringa @serukamba ameongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Iringa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mufindi. Aidha Mkurugenzi wa Mji Mafinga na Wakuu wa Idara walihudhuria Kikao hicho katika Ofisi ya Soko Kuu Mafinga Katika Halmashauri ya Mji Mafinga.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Mkuu wan Kitengo Cha Mawasiliano Serikali- Mafinga TC
@serukamba
@salekwalinda
@ortamisemi
@mohamed_mchengerwa
@clementsanga
@habari_digital
@msemajimkuuwaserikali
@maelezonews
@ccmtanzania
@ikuluhabari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.