Shule ya Sekondari Nyamalala inayopatikana katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga imefanya Mahafali ya kwanza ya Wanafunzi kuhitimu Elimu ya Kidato Cha Nne katika Viwanja vinavyopatikana katika Eneo hilo la Shule.
Afisa Elimu Sekondari Ndugu Stephen Shemdoe ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo amewapa hongera Wanafunzi kwa kuhitimu Kidato Cha Nne na amewasihi kuwa na Nidhamu na waepuke makundi yanayoweza kuwashawishi kufanya Matendo Mabaya katika Jamii.

“Serikali imetenga Fedha Shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuendeleza Ujenzi wa Shule hivyo ni Wajibu wenu Viongozi wa Shule kuhakikisha Fedha zinatumika ipasavyo pia nawaahidi kuwaletea Meza na Viti 80 kwa ajili ya Wanafunzi” amesisitiza Ndugu Shemdoe.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyamalala Ndugu Ezekieli Mwakalomba akisoma Risala ya Shule kwa Mgeni Rasmi amesema Shule hiyo ilianzishwa Mwaka 2006 ikiwa chini ya Shirika la Elimu Mufindi (MET) na ilipofika Mwaka 2021 Shule hiyo ilikabidhiwa Rasmi Serikalini chini ya Halmashauri ya Mji Mafinga na ilipofika Januari 2022 Shule ilidahili Rasmi Wanafunzi wa Kidato Cha Kwanza ikisimamiwa na Serikali na Wanafunzi waliohitimu ndiyo waanzilishi wa Shule ikimilikiwa na Serikali.
“Shule ina Watumishi 22 wote Wakiwa Walimu wa kudumu wa Kiume 12 na wa kike 10 pia wapo Walimu wa Kujitolea 4, wa Kiume 1 na wa kike 3 pia Shule ina Mlinzi 1 na Wapishi 2 kwa ajili ya chakula Cha mchana Cha Wanafunzi,pia Wanafunzi waliopo Kidato Cha Kwanza Hadi Cha Nne Jumla Yao ni 813 Wavulana 398 na Wasichana 415, Shule ni ya Kutwa kwa Kidato Cha Kwanza Hadi Cha Nne na Wanafunzi waliohitimu Jumla Yao ni 144 Wavulana 66 na Wasichana 78.”amesisitiza Ndugu Mwakalomba.

Vedasto Faustine Malima
Afisa Habari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.