Watumishi kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI Wametembelea katika Ofisi ya Halmashauri ya Mji Mafinga na kufanya kikao kazi kuhusu ujazaji wa dodoso kwa Watumishi wa Idara mbalimbali kwa lengo la kupata maoni ambayo yatawasaidia katika Utendaji wa Kazi.

Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Idara ya Utumishi ndugu Charles Mwaitege amesema Wageni wamefika kwa Lengo la kufanya Tathmini kupitia Dodoso Mtakazojaza kutoka Idara na Vitengo mbalimbali kwa lengo la kupata maoni ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali hivyo lazima ifanyike Tathmini ili kujua changamoto au mapungufu na kutafuta njia za kutatua hizo changamoto.

“Watumishi wote kutoka Idara na Vitengo mbalimbali hakikisheni mnasoma Dodoso vizuri na kuzijaza kwa usahihi ili kusaidia utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Raisi TAMISEMI”. amesisitiza.
Naye Afisa Takwimu kutoka TAMISEMI Bi; Elgiva Florence amesema Wanapima mafanikio ya Utendaji Kazi kwa kila Idara na Kitengo kupitia Takwimu mbalimbali ambazo Wanazikusanya kutokana na maoni kwa sababu zinaonyesha uhalisia wa Utendaji Kazi kutoka Halmashauri zote pia zinawasaidia kupata njia sahihi za kutatua changamoto mbalimbali.

Pamoja na hayo Afisa Uchumi kutoka TAMISEMI Ndugu Erick Myinga amesema kupitia Dodoso mbalimbali wanapima Utendaji na changamoto zinazopatikana katika Halmashauri pia Wanafanya Jitihada za kutatua hizo changamoto ili kuleta mabadiliko chanya ya Utendaji wa Kazi pia wanaonyesha Uhalisia wa Ushirikiano katika kazi.
Vedasto Faustine Malima
Afisa Habari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.