TASAF III YACHANGIA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 22 SHAMBA LA MITI EKARI 11 KIJIJI CHA ITIMBO KUPITIA WANUFAIKA WA TASAF
Posted on: May 12th, 2025
“ TASAF inashiriki moja kwa moja shughuli za Jamii ambapo wanufaika wa TASAF wanatakiwa kushiriki shughuli za kijami ili kuweza kujiinua kiuchumi.”
Katika Shamba hili walioshiriki Kazi ni wanufaika 41 Kutoka Kijiji cha Itimbo Kata ya Rungemba ambao walilipwa ujira zaidi ya shilingi milioni 17 .8 na TASAF ikanunua Miche yenye thamani ya shilingi milioni 4.5 pamoja na vifaa”
Akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi MJI Mafinga Bi. Fidelica Myovella alipotembelea na kufanya ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo, Mratibu wa TASAF Halmashauri ya MJI Mafinga Ndugu Leonard Irira amesema fedha hizo zimetumika kuwalipa wanufaika 41 kwenye shamba hilo la kijiji linalomilikiwa na Serikali ya Kijiji ambapo wanufaika huwa wanafanya kazi humo na kulipwa ujira.
Bi Myovella amesema Lengo la Serikali ni kuona Mpango unawanufaisha walengwa na wakihitimu basi wanatoka kwenye Mipango na kuendelea kujitegemea kiuchumi. Hivyo ameuomba Uongozi wa Serikali ya Kijiji kuhakikisha Shamba linakuwa safi muda wote ili thamani ya Fedha zilizowekwa na uhalisia uwe sawa.
Mkurugenzi MJI Mafinga ameongozana na Baadhi ya Wakuu wa Idara katika Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo.