Timu ya Uratibu wa Mwenge Mkoa wa Iringa imefanya ziara katika Halmashauri ya Mji Mafinga kushauri, kukagua, Miradi itakayopitiwa na mwenge wa Uhuru 2025 ambapo kwa Halmashauri ya Mji Mafinga Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa tarehe 1/5/2025 .
Timu hiyo ya Uratibu ya Mkoa wa Iringq imepokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mji Mafinga Ndugu, Peter Ngusa na Mratibu wa Mwenge Halmashauri ya Mji Ndugu Henry Kapella ambapo jumla ya miradi ya maendeleo 6 imepitiwa na kamati hiyo na Ushauri kutolewa.
Mwaka 2024 Halmashauri ya Mji Mafinga Kitaifa ilishika nafasi ya kwanza kikanda ikiongoza mikoa 4 yenye Halmashauri 27 na nafasi ya kwanza kwa mkoa wa Iringa.
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.