Halmashauri ya Mji Mafinga imepanga utaratibu wa upauaji wa majengo kwa kutumia mabati ya rangi mbalimbali ili kuboresha muonekano wa Mji na kurahisisha utambuzi wa maeneo katika Kata zote.
Akizungumza Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer amesema lengo ni kuboresha muonekano na utambuzi wa maeneo. Hivyo amewataka watendaji wa Kata zote 9 za halmashauri ya Mji Mafinga kuwajibika kutoa elimu kwa wananchi wanaojenga na watakaojenga katika Kata zao kuhakikisha majengo hayo mapya yanapauliwa kwa kutumia rangi iliyopendekezwa kutumika kwa kila kata.
Amefafanua kuwa kwa majengo ambayo yameshapauliwa hayatahusisha mpango huu, ila ikimpendeza mmiliki kubadili rangi ya paa atashauriwa kulingana na rangi za Kata husika.
Akizungumza Mhandisi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Christopher Nyamvugwa amesema kuwa ofisi ya ujenzi itakuwa wazi wakati wote kushirikiana na wananchi pale ushauri wa Kitaalamu unapohitajika na ofisi za kata kwaajili ya ufafanuzi zaidi.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
@angellah_kairuki
@halimadendego
@wizara_ya_ardhi
@ortamisemi
@daud_yasin_mlowe
@ccmmkoa_iringa
@ maelezo
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.