Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi; Fidelica Myovella amefanya Ziara ya kutembelea Miradi ya Ujenzi wa Shule za Sekondari na Msingi pamoja na Vituo vya Afya kwa lengo la kuangalia Jitihada na Uwajibikaji kwa Wasimamizi waliopewa dhamana ya kusimamia Miradi hiyo ya Ujenzi.
“Ongezeni juhudi katika kufanya kazi pia hakikisheni Miradi inakamilika kwa wakati pia Mafundi na Wasimamizi hakikisheni mnasimamia kikamilifu Utekelezaji wa Ujenzi kwa kila Mradi wa Shule au Kituo Cha Afya”. amesema Bi; Fidelica.
Pamoja na hayo Bi; Fidelica amewasihi Watendaji wa Kata na Vijiji kushirikiana na Madiwani katika kusaidia Utekelezaji wa Ujenzi wa Miradi ya Serikali pia Maafisa Kilimo wawasajili Wakulima kwa ajili ya kupata Pembejeo za Kilimo.
Akiambatana na Mkurugenzi katika Ziara hiyo Mkuu wa Idara ya Mipango Ndugu Peter Ngussa amesema Mafundi Wakuu wawe wanashirikisha Uongozi katika Kutoa Taarifa wanapohitaji Vifaa ili Miradi ikamilike kwa Wakati pia Mafundi wafanye Mgawanyo wa Kazi ili kurahisisha Utendaji.
Katika Ziara hiyo Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Sekta ya Elimu na Afya inaendelea kwa kishindo katika Halmashauri ya Mji Mafinga ikisimamiwa kikamilifu na Mkurugenzi,Watendaji na Wataalamu kutoka Vitengo mbalimbali hivyo Jitihada na Ushirikiano huo unasaidia katika Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Serikali.
Vedasto Faustine Malima
Afisa Habari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.