WAHESHIMIWA MADIWANI WAPITIA MPANGO KABAMBE WA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA KWA MIAKA ISHIRINI (2020-2040)
Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani kikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Mji wa Mafinga Mheshimiwa Julist Kisoma kimeketi leo na kupitia Mpango Kabambe wa Mji wa Mafinga kuanzia kwa mwaka 2020-2040.
Akimkaribisha Makamu Mwenyekiti Kufungua kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer amesema mpango huu ulianza kuandaliwa tangu mwaka 2017 ambao ulishirikisha wadau mbalimbali wa Kata zote ambapo walishauri yatengwe maeneo ya Mazishi, hifadhi za barabara na kilimo cha kisasa.
Mheshimiwa Julist Kisoma amepongeza Menejimenti ya Mji Mafinga kwa kazi nzuri ya Kuandaa mpango huo ambao utapanga Mji kwa miaka 20 ijayo kwani utakuwa ni Dira kubwa kwa Maendeleo ya Mji wa Mafinga ambao unakua kwa kasi kubwa.
Akiwasilisha Mpango huo kwa waheshimiwa Madiwani, Afisa Ardhi na Maliasili Bwana Rajabu Bogwa amesema vipaumbele saba vilivyopendekezwa na wadau ni pamoja na :-
Mpango Kabambe ni mpango wa kuongoza na kusimamia Uedelezaji na kudhibiti Ukuaji wa Mji/ Miji, ambapo mpango huu ulianza kuandaliwa tangu mwaka 2017, ambapo mnamo tarehe 5/9/2017 ulifanyika mkutano wa Wadau kwaajili ya Uandaaji wa Mpango huo kabambe ambapo mkutano ulifanyika katika ukumbi wa CCM wilaya ya Mufindi.
Baada ya Mpango huu kupitishwa na Kikao cha wadau, ngazi ya kata, Baraza la Madiwani na sasa unatarajiwa kuwasilishwa kwa Katibu Tawala Mkoa wa Iringa na Baadae kuwasiliswa Wizarani kwa hatua zaidi.
IMEANDALIWA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO- MAFINGA TC
SIMA BINGILEKI
AFISA HABARI MKUU
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.