Watumishi wa Ajira Mpya katika Halmashauri ya Mji Mafinga Wamepewa Mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki (MUKI) ili kuwawezesha kujifunza Sheria na Taratibu za Utumishi wa Umma pia kupata Vyeti vitakavyowasaidia kuthibitishwa Kazini.
Akiratibu Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Afisa Tehama Ndugu Benedict Kibiki amewasisitiza Watumishi hao kuzingatia utekelezaji wa Majukumu yao, Kufanya kazi kwa bidii na kutimiza Wajibu wao wakizingatia Sheria na Taratibu zilizowekwa.

" Kama Mtumishi wa Umma unatakiwa kujua upo wapi,na unafanya Nini na kwa Wakati gani,Kuna vitu unatakiwa uongee na vipo ambavyo hautakiwi kuongea kwa kufanya hivyo Taasisi itaheshimika" amesema Ndugu Kibiki.
Pamoja na hayo Afisa Utumishi Ndugu Julius Mwalongo amesema Mafunzo hayo yatawasaidia Watumishi wa Kada zote kufahamu masuala ya Kiutumishi na kutambua Serikali za Mitaa na Huduma zinazotolewa ili Kuboresha Utoaji wa Huduma kwa Wananchi.

Mfumo wa MUKI unaratibiwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Chuo Cha Serikali za Mitaa (LGTI) lengo kuu ni kutoa Mafunzo ambayo yatawasaidia Watumishi wote wa Ajira Mpya kuzingatia vyema Majukumu yao.
Vedasto Faustine Malima
Afisa Habari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.