SEKTA YA MIFUGO
Miundombinu ya Mifugo Majosho:
Halmashauri ya mji ina majosho 14 (9 ni ya vikundi nayo ni Josho la Kitelewasi,Josho la Kikombo,Josho la Isalavanu,Josho la Wambi,Josho la Mtula Josho la Ihefu,Josho la Itimbo (bovu) Josho la Sohill kijijini (Halijakamilika) Josho la matana na 5 ni ya taasisi). Majosho yanayo fanya kazi ni 9, mabovu ni kabisa 2 na yasiyo fanya kazi ni 3.
Hakuna malambo kwa ajili ya matumizi ya mifugo napia vibanio vya kudumu kwa ajili ya kutolea chanjo na huduma nyinginezo za mifugo hakuna. Uogeshaji mkubwa wa mifugo hufanywa kwa kutumia majosho na umewezesha kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa ya kupe kutoka asilimia 25 mwaka 2015 hadi asilimia 2 desemba 2017.
Aidha Halmashauri ina jumla ya machinjio 2 ambazo zipo kata za Boma na Changarawe machinjio ya kata ya Boma ni ya zamani kwasasa haifanyi kazi machinjio ndogo ya ng’ombe ipo Moja mtaa wa Ihefu. Halmashauri pia ina makaro 23 kwa ajili ya kuchinjia Nguruwe ambayo yapo kwenye kata za Boma, Changarawe,Upendo na Kinyanambo.
Halmashauri ina minada mmoja uliyopo Kata ya Isalavanu uitwao Lugoda Lutali, Kwa kipindi cha 2015 hadi Desemba mosi 2017 jumla ya ng’ombe 5948 Mbuzi 124 Kondoo 3 Nguruwe 76 wenye thamani ya Sh 3,770,052,000/= waliuzwa kupitia mnada huo.
Mnada huo ambao ni wa awali (Primary livestock market) umeingizwa katika mfumo wa kupashana taarifa za masoko ya mifugo nchini (Livestock Information Network Knowledge – LINK) unaosimamiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara na hivyo taarifa za mwenendo wa bei ya ng’ombe mnadani kwa madaraja hutolewa na kutangazwa nchi nzima kila wiki. Pia taarifa hiyo inapatikana katika mtandao wa simu za mkononi.
Magonjwa na Chanjo ya kuzuia magonjwa ya Mifugo
Magonjwa makuu yanayoathiri mifugo katika Halmashauri ni magonjwa yasababishwayo na kupe, chambavu, mdondo wa kuku na kichaa cha mbwa. Katika kipindi cha Julai 2015/16 hadi Novemba 2017, jumla ya kuku 361,461 wamechanjwa dhidi ya ugonjwa wa mdondo hii nipamoja na chanjo ya marudio, ng’ombe 13746 wamechanjwa dhidi ya ugonjwa wa chambavu. Aidha kwa kipindi cha kuanzia Julai 2015 hadi Novemba 2017, Jumla ya Mbwa2168 wamechanjwa dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Uhamilishaji wa Mifugo (Artificial Insemination).
Jumla ya ng’ombe 243 walihimilishwa na jumla ya ng’ombe 158 walishika mimba na kuzaa kati ya ng’ombe 85 walirudiwa. Halmashauri kwas asa haina vifaa vya uhimilishaji,na kwas asa uhimilishaji unafanywa na wataalamu wa shamba la mifugo Saohil, ununuzi wa vifaa vya uhimilishaji nimoja ya vipau mbele vyaidara kwenye bajeti ya 2018/2019.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.