Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmshauri ya Mji wa Mafinga umepitia jumla ya miradi nane ikiwa ni utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji Mafinga, ikishirikiana na wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Mradi ulifunguliwa ni mmoja na kuzindua miradi mitano na kukagua miradi miwili na kuweka jiwe la msingi mradi mmoja.
Thamani ya miradi yote ni tshs. bilioni, 1.7ambapo mchanganuo wa gharama za miradi yote nane Serikali Kuu imechangia tsh milioni 700.4, Halmashauri ya Mji Mafinga tshs. milioni 47.2 wahisani tsh milioni 38 na wananchi wamechangia nguvu kazi na fedha taslimu zenye thamani ya tsh milioni 954.5, miradi hii yote ipo katika sekta ya Elimu Afya, Maji,Kilimo, Mazingira na Ujenzi.
Katika miradi hiyo Mwenge umefungua mradi wa ujenzi wa daharia/hosteli ya wasichana shule ya sekondari mnyigumba, umezindua mradi wa kusaidia kuhifadhi na kutunza mazingira(WF Renuable Resource) uliopo katika kijiji cha rungemba, umezindua ujenzi wa tanki la maji mtaa wa tanganyika, umezindua klabu ya wapinga rushwa shule ya sekondari JJ Mungai, umezindua Mnara wa kumbukumbu ya kuuenzi Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, umezindua zahanati ya Nipende katika mtaa wa Amani.
Aidha umeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa Shule ya sekondari ihongole, pia umekagua mradi wa kilimo cha zao la parachichi mtaa wa ndolezi na mwisho kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Changarawe Matanana-Kisada yenye urefu wa kilometa 15 katika mradi huu kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Charles Francis Kabeho ametoa maelekezo ya kurudia kupima kwa ufanisi kama mkandarasi ametekeleza viwango vilivyowekwa katika mkataba ikiwa ni kwa lengo la kusimamia ubora wa barabara.
Akitoa ujumbe wa Mwenge kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ndugu Charles Francis Kabeho aliwahamsisha wananchi kuwekeza katika elimu chini ya ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 isemayo “ELimu ni Ufunguo wa Maisha Wekeza Sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu”
Kabeho aliendelea kuhamasisha kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya ukimwi na vvu, mapambano dhidi ya madawa ya kulevya na mapambano dhidi ya malaria.
Aidha alisistiza kwa viongozi wa serikali/uuma kufuatilia kwa makini miradi inayojengwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ijengwe kwa ubora unaotakiwa ili thamani ya pesa inayotumika ionekane “watumishi wote mnatakiwa kutimiza wajibu wenu katika kulitumikia Taifa letu”alisema Kabeho.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe Jamhuri William kupitia risala ya Utii wa Mwenge wa Uhuru 2018 Kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu utekekelezwaji wa maagizo ya Serikali katika sekta mbalimbali ikiwemo uanzishwaji wa viwanda, usimamizi wa mbolea ya ruzuku, kuokoa mifumo ya kiikoljia ya bonde la mto ruaha mkuu na walimu kutojihusisha na michango ya wazazi mashuleni .
Mwenge wa Uhuru uliwashwa rasmi na Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa tarehe 02 Aprili 2018 katika Mkoa wa Geita na unatarajiwa kumaliza mbio zake katika siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na wiki ya vijana Kitaifa tarehe 14 Oktoba 2018 mkoani Tanga.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.