Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo
Kilimo ni shughuli kuu ya kiuchumi katika Mji wa Mafinga imeweza kuajiri asilimia 70 na inatoa kipato kwa asilimia 80 ya wakazi. Mji wa Mafinga unazo Hakta 652,630 ambayo ni asilimia 92 ya hacta 712,300 zinazofaa kwa kilimo
Uwekezaji katika sekta ya Misitu
Katika Mji wa Mafinga kuna uwekezaji katika Shamba la Serikali kuna viwanda na vivutio vitatu vya utalii (MapangoyaUlole, Kaburi la chifu Mnyigumba n Kikundi cha wanawake cha Ufinyanzi Rungemba) ambavyo vimetambuliwa na kufanyiwa tathmini, jitihada za kuvitangaza vyanzo hivi inaendelea na endapo vingeboreshwa vingeweza kuwa vivutiovizuri vya utalii hapa mjini Mafinga na taifa kwaujumla. Halmashauri ya mji kwa kushirikiana na wataalam kutok aHalmashauri ya wilaya ya Mufindi na Mfukowamaendeleo ya jamii(TASAF) walitembelea vyanzo vya maji vya katika mitaa ya mkombwe, Ivambinungu,Pipeline, Igodi,Upendo, Changarawe vyanzo viwili, Ndolezi na timbo kwa kupima maeneo yanayozunguka vyanzo hivyo kwa kufanya makadilio ya vifaa na bajetinzima ya `mradi wa uhifadhi wa vyanzo vya maji ilikuweza kupanda miti rafiki na maji(Mivengi) kupitiamiradi ya kuhudumia kaya maskini, Sambamba na hilo katika kata ya kijiji cha Itimbo na Bumilayinga mradi wa upandaji miti umeshafanyiwa tathimini kwa kupima maeneo kwa ajili ya kutekelez amiradi hii. hamasishaji wa kujisajili ulifanyika katika kipindi cha robo ya kwanza kwa kushirikiana na wakala wa huduma za misitu Tanzania kwa kusambaza barua za kukumbusha kujisajili kufanya biashara ya mazaoi ya misitu kwa mwaka 2016/2017.
Utekelezaji wa Shughuli za Kilimo.
Sekta ya kilimo inachangia asilimia 50 ya pato la Mwananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga na pia inachangia katika utoaji wa ajira kwa asilimia 60.
Uzalishaji wa Mazao ya Chakula na biashara kwa msimu wa 2015/16.
i. Mazao ya Chakula: lengo lilikuwa kulima Ha 52,358 Na matarajio ya mavuno ilikuwa ni kuzalisha Tani 138,038.20, Hadi Juni 2014 Jumla ya Ha 45,258 zililimwa na mavuno halisi yalikuwa Tani 110,680.94.
ii. Mazao ya Biashara: lengo lilikuwa kulima Ha 198 Na matarajio ya mavuno ilikuwa ni kuzalisha Tani 198 Hadi Juni 2014 Jumla ya Ha 156 Zililimwa na mavuno halisi yalikuwa Tani 156.
Uzalishaji wa Mazao ya Chakula na biashara kwa msimu wa 2016/17.
i. Mazao ya Chakula: lengo lilikuwa kulima 50,344 Na matarajio ya mavuno ilikuwa ni kuzalisha Tani 127,262 Hadi Juni 2015 Jumla ya Ha 45,370 Zililimwa na mavuno halisi yalikuwa Tani 117,585.10
ii. Mazao ya Biashara: lengo lilikuwa kulima Ha 167 Na matarajio ya mavuno ilikuwa ni kuzalisha Tani 167 Hadi Juni 2015 Jumla ya Ha 150 Zililimwa na mavuno halisi yalikuwa Tani 150.
Ununuzi wa mazao ya biashara msimu wa 2016/17
Zao pekee la biashara katika eneola Halmashauri ya Mji niAlizeti ambapo jumla ya tani 150 zilizalishwa kwakuuzwa kwa Wafanyabiashara na Wasindikaji.
Malengo ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula na biashara kwa msimu wa 2017/18
i. Mazao ya Chakula: lengo ni kulima Ha 50,505.50 Na matarajio ya mavuno ni kuzalisha Tani 127,955.
ii. Mazao ya Biashara: lengo ni kulima Ha 156 Na matarajio ya mavuno ni kuzalisha Tani 156.
Pembejeo za Ruzuku ya Serikali
Hali ya Pembejeo kwa Msimu wa Kilimo wa mwaka 2016/2017
Halmashauri ya Mji wa Mafinga ni miongoni mwa Halmashauri 5 za Mkoa wa Iringa zilizopata mgao wa ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa msimu wa mwaka 2016/2017. Aidha Halmashauri ilipata ruzuku ya mifuko 2,040 ya mbolea ya kupandia, mifuko 2,040 ya mbolea ya kukuzia na mifuko 2,040 kwa ajili ya mbegu za mahindi chotara. Mgao wa Mifuko 2,040 ya ruzuku ya mbegu ya mahindi chotara kwa ajili ya kaya 2,040 za kilimo huku kila kaya ikipata mfuko 1 wa mbolea ya kupandia, 1 wa mbolea ya kukuzia na kilo10 za mbegu ya mahindi chotara vinavyotosha kuhudumia ekari moja. Hata hivyo mbegu ya ruzuku haikupatikana kutokana na kuchelewa kwa mchakato wa kupata makampuni ya mbegu.
Hadi kufikia tarehe Novemba jumla ya tani 102 kati ya tani 102 za mbolea ya kupandia, tani 102 kati ya tani 102 za mbolea ya kukuzia na mbegu tani 0 kati ya tani 20.4 za mbegu zilikuwa zimesambazwa katika vijiji/mitaa 23 vilivyonufaika na ruzuku hii ndani ya Halmashauri ya Mji wa Mafinga.
Hali ya Chakula katika Halmashauri,
Mavuno ya mazao ya Chakula kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2016/17 yalikuwa ni jumla ya tani 81,384.5 za nafaka (Mahindi na ngano) na tani 10,127 za mikunde (Maharage na Njegere. Mahitaji halisi ya chakula ni tani 21,492.3 za nafaka na tani 7,164.10 za mikunde na hivyo kuwa na ziada ya chakula tani 59,892.20 za nafaka na tani 2,962.9 za mikunde. Kwa misimu 2 mfululizo Halmashauri haijawahi kukumbwa na baa la njaa.
Mikakati ya Halmashauri ya kuhakikisha upatikanaji wa chakula
Halmashauri imeweka mikakati ifuatayo kuhakikisha kuwa kivutio cha bei hakitaathiri upatikanaji wa chakula:
i. Kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima
ii. Kuelimisha wakulima juu ya hifadhi ya chakula katika Kaya
iii. Kuelimisha Wakulima juu ya mahitaji ya chakula katika Kaya
Kilimo cha Umwagiliaji
Eneo linalofaa kwa Kilimo cha Umwagiliaji ni wastani wa hekta 790. Hadi sasa eneo linalomwagiliwa ni hekta 99 (Mtula hekta 75, Mlelwa hekta 16 na Ibikititu hekta 8) sawa 12.5%.
Hali ya matumizi ya zana bora za Kilimo
Halmashauri ya Mji wa Mafinga ina matrekta makubwa 8, matrekta madogo (power tiller) 30 na majembe ya kukokotwa na ng’ombe (plau) 810 vinavyotumika kwa ajili ya kilimo.
Huduma za Ugani
Halmashauri ya Mji wa Mafinga ina jumla ya Maafisa Ugani kilimo13 kati ya 29 wanaohitajika hivyo kuwa na upungufu wa maafisa ugani kilimo 16 na Kitengo cha Ushirika kina watumishi 3 kati ya 4 wanaotakiwa hivyo kuwa na upungufu wa Mtumishi 1.
Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Sekta ya Kilimo
Kwa mwaka 2016/2017 sekta ya Kilimo imetengewa Jumla ya Tshs. 100,000,000 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Kujengea (Lining) mfereji Mkuu – mradi wa umwagiliaji Mtula, Kuanzisha vishamba vya maonesho katika mradi wa umwagiliaji Mtula na Ujenzi wa Jengo la Maonesho ya Nanenane Mbeya.
HALMASHAURI YA MJI MAFINGA KUSHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE JIJINI MBEYA 2022
KARIBU NANE NANE MBEYA 2024 KATIKA BANDA LA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA
MKURUGENZI MJI MAFINGA NDUGU.FIDELICA MYOVELLA AKITEMBELEA BANDA LA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA
MKURUGENZI MJI MAFINGA AKIVALISHWA VAZI LA ASILI YA KIHEHE NA MMOJA WA WAJASILIAMALI KATIKA BANDA LA MJI MAFINGA-2024
MBOGA KICHUGUU KATIKA BANDA LA MJI MAFINGA.
MKUU WA MKOA WA NJOMBE MHESHIMIWA ANTHONY MTAKA AKIWEKA SAINI KATIKA BANDA LA MJI MAFINGA KATIKA MAONESHO YA 88 JIJINI MBEYA 2024
MWENYEKITI MJI MAFINGA MHESHIMIWA REGNANT KIVINGE AKIWA AMEAMBATANA NA MKURUGENZI MJI MAFINGA BI. FIDELICA MYOVELLA WAKIKAGUA BIDHAA KWENYE BANDA LA MJI MAFINGA 88 MWAKA 2024
WATUMISHI IDARA YA KILIMO NA MIFUGO KWENYE VAZI RASMI LA KILIMO(KOMBATI) LILILOTOLEWA NA WIZARA YA KILIMO
MOJA YA GREENHOUSE INAYOMILIKIWA NA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA IDARA YA KILIMO
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.