UTANGULIZI.
Halmashauri ya Mji Mafinga ilianzishwa mwaka 2015 ambapo mwanzoni ilikuwa sehemu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi. Halmashauri ya mji Mafinga ni miongoni mwa Halmashauri Tano za Mkoa wa Iringa ambazo ni Manispaa ya Iringa, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo. Halmashauri ya Mji Mafinga iko umbali wa Kilometa 80 kutoka Iringa mjini.
DIRA NA DHIMA YA HALMASHAURI.
Dira.
Halmashauri ya Mji wa Mafinga inapenda kuwaona wakazi wake wanaishi maisha bora na endelevu
Mwelekeo wa Halmashauri (Dhima).
Halmashauri ya Mji Mafinga kwa kushirikiana na wadau wa Ndani na Nje inatarajia kutoa huduma bora na endelevu kwa kuzingatia vipaumbele na raslimali zilizopo ifikapo mwaka 2025.
MIPAKA NA JIOGRAFIA YA HALMASHAURI YA MJI.
Halmashauri ya Mji Mafinga sehemu kubwa imezungukwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa upande wa kusini, Magharibi na Mashariki na Kaskazini imepakana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini. Mji wa Mafinga upo kati ya Latitude 80– 90Kusini na Logtude 35 - 36 Mashariki mwa Greenwich.
HALI YA HEWA
Halmashauri ya Mji mafinga inapata hali ya joto ya nyuzi 19 na karibu nyuzi 5 Kiwango cha Juu ni miezi ya Novemba na Desemba ambapo inakuwa na wastani wa nyuzi 28. Kiwango cha chini ni miezi ya Juni hadi Agost kuna nyuzi joto kati ya 11 na 22. Wastani wa hali ya unyevu ni 505 na inapungua kwa asilimia 33 Kwa ujumla wastani wa mvua ni kati ya milimita 452 kiwango cha chini na milimita 1,000 kwa mwaka.
ENEO LA HALMASHAURI
Halmashauri ya Mji wa Mafinga ina eneo la kilometa za mraba 953 kati ya hizo 936 ni eneo lanichi kavu na 17 ni eneo la maji. Aidha tarafa ya Ifwagi inaongoza kwa kuwa na eneo kubwa (asilimia 59.2), ikifuatiwa na tarafa ya Malangali (asilimia 26.2) na ya mwisho ni tarafa ya Sadani ambayo ni asilimia 14.6. Kata ya Ifwagi inalo eneo la maji asilimia 57.6, Malangali asilimia 25.9 na Sadani asilimia 16.5 kwa mchanganuo ufuatao;
Jedwali namba 1 Mgawanyo wa Eneo la Ardhi.
Tarafa
|
Kata
|
Eneo la Ardhi
|
Eneo la Maji
|
Jumla ya Eneo
|
Asilimia ya Ardhi
|
Asilimia ya Maji
|
|
Ifwagi
|
Boma
|
11.0
|
0.5
|
11.5
|
1.2
|
2.9
|
|
|
Wambi
|
2.5
|
1.4
|
3.9
|
0.3
|
8.2
|
|
|
Kinyanambo
|
58.5
|
1.0
|
59.5
|
6.3
|
5.9
|
|
|
Upendo
|
32.2
|
1.6
|
33.8
|
3.4
|
9.4
|
|
|
Saohill
|
195.6
|
2.1
|
197.7
|
20.9
|
12.4
|
|
|
Changarawe
|
20.1
|
0.2
|
20.3
|
2.1
|
1.2
|
|
|
Rungemba
|
234.3
|
3.0
|
237.3
|
25.0
|
17.6
|
|
Jumla Ndogo
|
|
554.3
|
9.8
|
564.1
|
59.2
|
57.6
|
|
Sadani
|
Isalavanu
|
137.0
|
2.8
|
139.8
|
14.6
|
16.5
|
|
Malangali
|
Bumilayinga
|
244.8
|
4.4
|
249.2
|
26.2
|
25.9
|
|
Jumla Kuu
|
|
936.0
|
17.0
|
953.0
|
100.0
|
100.0
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Chanzo: Ofisi ya Mkurugenzi Mji.
Halmashauri ya Mji Mafinga ina jumla ya Tarafa 3, Kata 9, Vijiji 11, Vitongoji 49, Mitaa 30,kwa mchanganuo ufuatao:-
Jedwali Namba 2 Mgawanyo wa eneo la Utawala.
Tarafa
|
Kata
|
Vijiji
|
Mitaa
|
Vitongoji
|
Ifwagi
|
Boma
|
0
|
6
|
0
|
|
Wambi
|
0
|
4
|
0
|
|
Kinyanambo
|
0
|
5
|
0
|
|
Upendo
|
0
|
5
|
0
|
|
Saohill
|
0
|
5
|
0
|
|
Changarawe
|
0
|
5
|
0
|
|
Rungemba
|
3
|
0
|
13
|
Jumla Ndogo
|
|
11
|
20
|
49
|
Sadani
|
Isalavanu
|
4
|
0
|
16
|
Malangali
|
Bumilayinga
|
4
|
0
|
20
|
Jumla Kuu
|
|
11
|
30
|
49
|
Chanzo: Ofisi ya Mkurugenzi Mji.
Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Uchaguzi 1
Waheshimiwa Madiwani wa Kuchaguliwa katika Kata 9
Waheshimiwa Madiwani wa Viti Maalumu 3
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012, Halmashuri ilikuwa na Kaya 14,208 na Wakazi wapatao 71,641 kati yao Wanaume ni 34,522 na Wanawake ni 37,119 (kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi, 2012). kwa sasa Halmashauri inakadiriwa kuwa na watu 87,761 wanaume 42,289 na wanawake 45,470 hii ni kutokana na ongezeko la asilimia 4.5 kwa mwaka.
Jedwali namba 3 Idadi ya watu
Halmashauri
|
Km za Mraba
|
Idadi ya watu
|
||
|
|
Me
|
Ke
|
Jumla
|
Mji wa Mafinga
|
953
|
34,522
|
37,119
|
71,641
|
Chanzo: Ofisi ya Mkurugenzi Mji.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI
Zaidi ya asilimia 91 ya wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga hutegemea Kilimo kwa kujiongezea kipato, ambapo hutegemea sana mauzo kutokana na mazao makuu ya Kilimo ambayo ni Miti ya Kisasa, Misitu ya Asili, Nafaka asilimia 0.7% ya kaya zote za Halmashauri hii zinafuga mojawapo ya wanyama kama Ng’ombe, Mbuzi na Nguruwe. Mchango wa kila sekta katika maendeleo ya uchumi ni kama ifuatavyo; Kilimo 91%, shughuli za biashara 1% watumishi (kazi za ofisini) 0.3%, ufugaji 0.7% na shughuli nyingine ndogo ndogo (Ujasiimali) 8%.
MIKAKATI YA HALMASHAURI KATIKA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO
Katika kipindi cha miaka miwili kuanzia Julai 2015 hadi Juni 2017, Halmashauri ilipanga kutekeleza malengo na mikakati mbalimbali ili kuondoa kero na kuboresha maisha ya Wananchi. Baadhi ya Mikakati hiyo ni pamoja na kutekeleza:-
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015
Mkakati wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, chini ya utaratibu wa mpango wa matumizi wa muda wa kati (MTEF).
Malengo endelevu ya milenia 2030
Matakwa ya Sera na sheria zinazosimamia sekta mbalimbali.
Mkakati wa kitaifa wa Kupambana na Kuzuia Rushwa.
Mkakati wa kupambana na UKIMWI.
Hotuba ya mh. Rais wakati wa kufungua bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma Novemba 2015.
Katika kuhakikisha mafanikio yanapatikana Halmashauri ya Mji imejiwekea mikakati ifuatavyo:-
Kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi yenye ufanisi mkubwa ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kutengeneza mazingira bora ya Utawala kwa kudumisha amani na umoja.
Kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwapatia ushauri wa kitaalamu.
Kuhakikisha tunaongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali kwa kuongeza ubora na kuuza kwa bei nzuri na hatimaye kuongeza kipato na pato la Taifa.
Kuhakikisha wadau mbalimbali wanashiriki katika shughuli za Maendeleo.
Kuandaa Mipango shirikishi na endelevu.
Kuboresha na kubuni vyanzo vya mapatoya Halmashauri
Ili kutekeleza mikakati hiyo ya Halmashauri Halmashauri inazingatia fursa mbalimbali zilizopo hapa Halmashaurini ikiwa ni pamoja na:
Watu: Rasilimali watu ndio msingi mkubwa wa mafanikio katika utekelezaji wa mipango yetu ya Maendeleo ambapo kwa takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Halmashauri ilikuwa na watu 45,349 Asilimia (63.3%) ya Idadi ya watu 71,641 waliokuwa na uwezo wa kufanya kazi.
Ardhi:Halmashauri ina rasilimali ya ardhi yenye rutuba ya kutosha ambayo inaweza kutumika kwa shughuli mbalimbali za kuinua uchumi. Hata hivyo eneo linalotumika kwa kilimo ni hekta 263,552 kati ya hekta 712,300 zinazofaa kwa kilimo.
Fursa za uwekezaji na viwanda:
Katika Mji wa Mafinga viwanda vilivyopo ni pamoja na kutengeneza mazao yatokanayo na kilimo viwanda vikubwa ni pamoja na Unilever Tea Tanzania Ltd, Mafinga Tea &Coffee Company, Tanzania Pyrethrum Processing & Marketing Company, Mafinga Paper Mills (MPM) na Chai Bora
Fedha: Rasilimali fedha kutoka serikali kuu, mapato ya ndani, michango ya wananchi na wadau wa maendeleo umewezesha Halmashauri kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na utoaji huduma muhimu za kijamii na kiuchumi.
Miundombinu: Miundo mbinu mizuri ya barabara na mawasiliano ambayo imewezesha kufanikisha shughuli za Maendeleo kwani asilimia 100% (416km) ya barabara zinapitaka mwaka mzima. Katika kushughulikia na kuondoa kero za wananchi. Halmashauri imekuwa ikitekeleza wajibu wake ikizingatia lengo kuu la kuchochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania na kupunguza umaskini kwa hususani wa hali ya chini:
11. MAFANIKIO YA HALMASHAURI KATIKA KUTEKELEZA SHUGHULI ZA MAENDELEO.
11.1 UKUSANYAJI WA MAPATO YA SERIKALI:
ii.Mapato ya Halmashuri kupitia Serkali kuu.
Katika kipindi cha 2015/2016 hadi 2016/2017Halmashuri iliendelea kupokea fedha kutoka serkali kuu na wahisani mbalimbali. Mwaka 2015/2016 kiasi kilichopokelelewa ni Sh. 4,967,651,887.76 wakati kiasi kilichopokelewa mwaka 2016/2017 kiasi kilichopokelewa ni Sh. 11,332,448,232.43. 2017/2018 Halmashuri imeidhinishiwa Sh. 14,149,859,800.00 ikiwa ni mishahara na matumizi ya kawaida. Hadi Novemba 2017 kiasi kilichopokelewa ni Sh. 4,691,650,800.00 toka serkali kuu na wahisani sawa na asilimia 33.1
iii. Hali ya makusanyo ya mapato ya Ndani hadi kufikia mwaka wa fedha 2017/2018
Makusanyo mwaka 2015/2016 kiasi kilichokusanywa ni Sh. 1,183,245,036.00 toka mwaka 2015/2016 hadi kufikia Sh. 1,625,551,884.00 Mwaka 2017/2018 Halmashuri imekadiria kukusanya kiasi cha Sh. 3,120,869,000.00 hadi kufikia mwezi novemba 2017 kiasi kilichokusanya ni Sh. 912,824,213.14 sawa na asilimia 29.25
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.