MIKAKATI YA HALMASHAURI KATIKA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO
Katika kipindi cha miaka miwili kuanzia Julai 2015 hadi Juni 2017, Halmashauri ilipanga kutekeleza malengo na mikakati mbalimbali ili kuondoa kero na kuboresha maisha ya Wananchi. Baadhi ya Mikakati hiyo ni pamoja na kutekeleza:-
• Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015
• Mkakati wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, chini ya utaratibu wa mpango wa matumizi wa muda wa kati (MTEF).
• Malengo endelevu ya milenia 2030
• Matakwa ya Sera na sheria zinazosimamia sekta mbalimbali.
• Mkakati wa kitaifa wa Kupambana na Kuzuia Rushwa.
• Mkakati wa kupambana na UKIMWI.
• Hotuba ya mh. Rais wakati wa kufungua bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma Novemba 2015.
Katika kuhakikisha mafanikio yanapatikana Halmashauri ya Mji imejiwekea mikakati ifuatavyo:-
• Kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi yenye ufanisi mkubwa ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
• Kutengeneza mazingira bora ya Utawala kwa kudumisha amani na umoja.
• Kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwapatia ushauri wa kitaalamu.
• Kuhakikisha tunaongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali kwa kuongeza ubora na kuuza kwa bei nzuri na hatimaye kuongeza kipato na pato la Taifa.
• Kuhakikisha wadau mbalimbali wanashiriki katika shughuli za Maendeleo.
• Kuandaa Mipango shirikishi na endelevu.
• Kuboresha na kubuni vyanzo vya mapatoya Halmashauri
Ili kutekeleza mikakati hiyo ya Halmashauri Halmashauri inazingatia fursa mbalimbali zilizopo hapa Halmashaurini ikiwa ni pamoja na:
Watu: Rasilimali watu ndio msingi mkubwa wa mafanikio katika utekelezaji wa mipango yetu ya Maendeleo ambapo kwa takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Halmashauri ilikuwa na watu 45,349 Asilimia (63.3%) ya Idadi ya watu 71,641 waliokuwa na uwezo wa kufanya kazi.
Ardhi:Halmashauri ina rasilimali ya ardhi yenye rutuba ya kutosha ambayo inaweza kutumika kwa shughuli mbalimbali za kuinua uchumi. Hata hivyo eneo linalotumika kwa kilimo ni hekta 263,552 kati ya hekta 712,300 zinazofaa kwa kilimo.
Fursa za uwekezaji na viwanda:
Katika Mji wa Mafinga viwanda vilivyopo ni pamoja na kutengeneza mazao yatokanayo na kilimo viwanda vikubwa ni pamoja na Unilever Tea Tanzania Ltd, Mafinga Tea &Coffee Company, Tanzania Pyrethrum Processing & Marketing Company, Mafinga Paper Mills (MPM) na Chai Bora
Fedha: Rasilimali fedha kutoka serikali kuu, mapato ya ndani, michango ya wananchi na wadau wa maendeleo umewezesha Halmashauri kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na utoaji huduma muhimu za kijamii na kiuchumi.
Miundombinu: Miundo mbinu mizuri ya barabara na mawasiliano ambayo imewezesha kufanikisha shughuli za Maendeleo kwani asilimia 100% (416km) ya barabara zinapitaka mwaka mzima. Katika kushughulikia na kuondoa kero za wananchi. Halmashauri imekuwa ikitekeleza wajibu wake ikizingatia lengo kuu la kuchochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania na kupunguza umaskini kwa hususani wa hali ya chini
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.