IDARA YA AFYA
MKUU WA IDARA: DKT BONAVENTURA CHITOPELA
Idara ya Afya ni miongoni mwa idara katika Halmashauri ya Manispaa ya Mji Mafinga. Idara ya Afya inatekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo mbalimbali inayotolewa na Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Huduma hizi zimekuwa zikitolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya na kwa njia ya mkoba katika maeneo mbalimbali ya Manispaa. Katika Halmashauri ya Manispaa ya Mji Mafinga kuna jumla ya vituo 45 vya kutolea huduma za afya. Vituo hivi vinamilikiwa na serikali, watu binafsi, mashirika ya dini pamoja na taasisi za serikali. Vituo vya kutolea huduma za Afya vinavyomilikiwa na serikali ni 15, Vituo 21 vinamilikiwa na watu binafsi, 4 vinamilikiwa na mashirika ya dini na vituo 5 vinamilikiwa na taasisi za serikali. Kati ya vituo hivyo 45, kuna hospitali 1, vituo vya Afya 12 na zahanati 32.
MAJUKUMU YA IDARA
Idara ya Afya inatekeleza majukumu makuu mawili abayo ni Afya kinga na Afya tiba. Kupitia Afya tiba idara imelenga kutoa matibabu sahihi kwa gharama nafuu kwa wananchi wa Manispaa ya Mji Mafinga pamoja na Wilaya za jirani. Afya kinga imelenga kuwakinga wananchi wasipate magonjwa yale ya kuambukiza, yasiyoyakuambukiza pamoja na kuzuia magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.
AFYA TIBA
Idara imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na kutekeleza mpango mkakati wa afya wa mwaka 2015 -2020. Katika kuhakikisha wananchi wanapata tiba sahihi, idara imekuwa ikitekeleza majukumu yafuatayo:
Kusimamia manunuzi ya dawa, vitendanishi vya maaabara ,vifaa na vifaa tiba kisha kuvisambaza kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Kutoa huduma za matibabu na uuguzi kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya zikiwemo huduma za upasuaji mkubwa na mdogo. Huduma hizi ni kwa wagonjwa wa nje na wagonjwa wa kulazwa.
Kufanya ukaguzi wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya
Kusajili na kuhuisha maduka ya dawa na vipodozi, kuyafanyia ukaguzi mara kwa mara na kuhakikisha yanafuata sheria, kanuni na miongozo inayosimamia uanzishaji na uwepo wa maduka hayo
Kusimamia pamoja na kuzikagua maabara zote na kuhakikisha zimesajiliwa na zinatoa huduma bora kulingana na miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya.
Kutoa, kusimamia na kuratibu huduma za afya ya uzazi na mtoto katika Manispaa . Huduma hizi ni pamoja na uzazi salama, huduma za uzazi wa mpango, huduma za chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito, uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti. Huduma nyinginezo ni pamoja na huduma za kuzuia ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.
Kuratibu huduma za kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na UKIMWI. Huduma zitolewazo ni pamoja na matibabu na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, huduma za kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto, huduma za kuchunguza na kutibu magonjwa ya ngono pamoja na huduma za wagonjwa majumbani. Huduma hizi hutolewa katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
AFYA KINGA
Idara imeendelea kutekeleza majukumu mbalimbali yanayolenga kuwakinga wananchi na magonjwa ya kuambukiza. Mojukumu hayo ni pamoja na:
Ukaguzi wa nyumba za kuishi na majengo ya biashara kama vile nyumba za kulala wageni,majengo ya kutengeneza na kuuza vyakula ili kuondoa machukizo yanayoweza kuhatarisha afya ya binadamu.
Utoaji wa elimu ya afya kwa umma kuhusu masuala mbalimbali ya afya.
Utoaji wa chanjo kwa magonjwa ya kuambukiza kwa wajawazito na watoto
Usimamizi wa afya na usalama mahala pa kazi
Usimamizi wa usafi wa Mazingira.
KITUO CHA AFYA UPENDO.
UKARABATI WA WODI NAMBA 5 KATIKA HOSPITALI YA MJI MAFINGA
UKARABATI UMEKAMILIKA:
MILIONI 25- KUTOKA SERIKALI KUU
MILIONI 8- MAPATO YA NDANI
JENGO LA KUTOLEA HUDUMA ZA DHARURA(EMD) HOSPITALI YA MJI MAFINGA- LIMEKAMILIKA NA LINATUMIKA
KITUO CHA AFYA BUMILAYINGA- JENGO LA OPD LINATUMIKA- UJENZI MAJENGO MENGINE UNAENDELEA
DC- MUFINDI DKT. LINDA SALEKWA ATEMBELEA UJENZI WA JENGO LA KUHIFADHIA MAITI LINALOJENGWA KATIKA HOSPITALI YA MJI MAFINGA.
NYUMBA YA WATUMISHI KATIKA ZAHANATI YA KISADA UJENZI UMEGHARIMU KIASI CHA SHILINGI MILIONI 60 KUTOKA MAPATO YA NDANI YA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA.
DC MUFINDI MHESHIMIWA DKT LINDA SALEKWA AKIWA NA MKURUGENZI MJI MAFINGA BI, FIDELICA MYOVELLA KWENYE ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA ZAHANATI YA KISADA
UJENZI WA WODI YA DARAJA LA KWANZA KATIKA HOSPITALI YA MJI MAFINGA UNAENDELEA-
UJENZI WA JENGO LA KUFULIA NGUO UMEKAMILIKA KATIKA KITUO CHA AFYA BUMILAYINGA.
MAPOKEZI YA GARI LA KUBEBA WAGONJWA KATIKA KITUO CHA AFYA IFINGO- LILILOKABIDHIWA KATIKA KITUO HICHO NA MBUNGE WA JIMBO LA MAFINGA MHESHIMIWA COSATO CHUMI
MKUU WA MKOA WA IRINGA MHESHIMIWA PETER SERUKAMBA AKIKAGUA UJENZI WA JENGO LA KUFULIA NGUO KATIKA HOSPITAL IYA MJI MAFINGA
JENGO LA KUFULIA NGUO KATIKA HOSPITALI YA MJI MAFINGA.
JENGO ,LA KUHIFADHIA MAITI(MOTUARY) KATIKA HOSPITALI YA MJI MAFINGA.
WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA KASSIM MAJALIWA MAJALIWA(MB) ALIPOTEMBELEA NA KUKAGUA MAJENGO KATIKA HOSPITALI YA MJI MAFINGA 2024.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.