Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt Linda Selekwa ameendesha kikao cha tathimini ya viashiria vya mkataba wa lishe ngazi ya Kata, Mitaa na Vijiji kwa kipindi cha robo ya tatu januari hadi machi 2025 na robo ya nne aprili hadi june 2025 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga.
Katika kikao hicho Dkt Linda Selekwa ametoa rai kwa Maafisa Lishe kwa kushirikiana na idara ya elimu kuhakikisha wanahamasisha idadi ya wanafunzi wanaokula chakula shuleni kwa Kata zote za Halmashauri ya Mji Mafinga hatua hii itasaidia kukuza ufaulu wa watoto na kupunguza utoro mashuleni na utapia mlo kwa watoto, pia ameagiza kuwe na motisha ambayo inatengwa kwa wahudumu wa afya ya msingi na wa mama wajawazito ambao wamefanya vizuri kufatilia shughuli za lishe.
Aidha Dkt Linda Selekwa ameagiza wahudumu wa afya ya msingi kuwa wanatembelea wananchi ili kugundua watoto wenye changamoto za lishe ili waweze kutibiwa na kupewa elimu ya lishe hatahivyo ametoa rai kuzingatia maazimisho ya lishe katika mitaa na vijiji vyote ili kuweza kutoa elimu kwa walengwa pia watendaji wa Kata wahakikishe wanawatambua watoto wenye changamoto katika maeneo yao na Kamati za Kata ziwe na ajenda ya kudumu ya afya hususa kwenye masuala ya lishe.
Michael Ngowi – Afisa Habari
Wajumbe wa kikao cha Lishe wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mfundi Dkt Linda Selekwa juu ya mambo mbalimbali .
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.