Halmashauri ya Mji Mafinga kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imeendesha mafunzo kwa vikundi ambavyo vinanufaika na mikopo ya asilimia kumi mafunzo hayo yamelenga namna ya kufanya biashara na kuongeza thamani ya bidhaa ili mikopo watakayopewa iwe na tija na kuwainua kiuchumi katika mafunzo hayo ambayo yamejumisha vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye walemavu mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Mufindi.
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji Mafinga Bi Fedelica Myovela ametoa rai kwa vikundi vyote vya wanufaika wa mikopo kuhakikisha wanasimamia malengo yao ambayo wameyapanga, na pia kuhakikisha wanatumia wataalamu waliopo katika shughuli zao Halmashauri inawataalamu wote wa biashara, kilimo na mifugo ili kuwapa mafunzo na kuendesha miradi kitaalamu lengo la serikali ni kuhakikisha inawainua wananchi kiuchumi.
Mafunzo hayo ambayo yametolewa kwa vikundi 26 kutoka Kata zote za Halmashauri ya Mji Mafinga ambavyo vimepatiwa mafunzo mbalimbali ikiwemo ya kuongeza thamani ya bidhaa ambazo wanazalisha ili kuhakikisha wanawafikia wateja na kukuza mitaji yao na kuongeza mauzo ,pia wamepewa mafunzo ya kutumia teknolojia mpya ambazo zimekuwa zikisaidia kuongeza ufanisi na kupunguza gharama katika uzalishaji wa bidhaa zao hata hivyo wamekumbushwa kutoa huduma bora kwa wateja wao ili kuweza kumudu soko na ushindani uliopo katika biashara na ujasiriamali.
Katika mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Elias Msuya amesema lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo uwezo na ufanisi wanufaika wote namna ya kusimamia mikopo yao ili kuepuka anguko la kibiashara au kutozalisha jambo litakalowezesha kurejesha na kumaliza mikopo.
Aidha Afisa Mipango Ndugu Piter Ngusa amewaeleza wanufaika wa mikopo hiyo kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya fedha na vitu wanavyofanya na pia kuepuka kuanzisha miradi mipya ambayo wajaipanga jambo litakalopelekea kushindwa kurejesha mikopo waliyopatiwa pia kuhakikisha wanatumia wataalamu.
Michael Ngowi Afisa Habari.
Baadhi ya wanufaika wa mikopo ya asilimia kumi wakiendelea kupata mafunzo kutoka kwa wataalamu mbalimbali.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.