Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga kutoka katika Idara ya Utumishi na Maliasili wamefanya ziara katika ofisi ya serikali ya Mtaa wa Isalavanu na Kutoa Elimu kwa Wakazi hao kuhusu Utawala Bora na Utunzaji wa Mazingira.
Akiongea na Wakazi hao katika ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Isalavanu Afisa Utumishi ndugu Dennis Mselema amesema “Wananchi ni haki yenu kuelewa Utawala Bora kwa sababu inawasaidia kutambua demokrasia na haki zenu za msingi,pia Mtendaji na Mwenyekiti ni vyema kufanya vikao vya Mkutano Mkuu kila baada ya miezi mitatu ili kujua Mapato na Matumizi ya Serikali ya Mtaa na kila Mwananchi ana wajibu wa kulinda Mali ya Umma”.
Naye Afisa Maliasili Ndugu Demitrus Kamtoni amesema kuwa Wananchi wanapaswa kutunza Mazingira kwa kuepuka Kukata Miti bila Vibali na Utaratibu wa utoaji wa Vibali unapaswa kufuatwa kwa kila Mwananchi anayehitaji kuvuna shamba lake pia atakayebainika kukiuka Utaratibu Atatozwa Faini ya Shilingi Elfu Hamsini. “Wananchi pia ni wajibu wenu kutunza Vyanzo vya Maji kwa kwa kufanya shughuli za kilimo umbali wa Mita sitini kutoka vyanzo cha Maji,Pia kuhusu
Shughuli za Uchimbaji Wa Madini lazima Taarifa itolewe kwenye Ofisi ya Mkurugenzi na utoke uthibitisho kutoka Ofisi ya Madini ya Mkoa wa Iringa pia ni vyema Wananchi kuunda Kikundi Cha Kuvuna Nyuki kwani watapata faida kubwa kwa sababu ya uwepo mkubwa wa Soko la Asali na Nta.”
Amesema. Wakati huo huo Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Isalavanu ndugu Bosco Mgimwa amesema Wanashukuru Halmashauri ya Mji wa Mafinga ikiongozwa na Mkurugenzi Bi, Fidelica Myovella kwa Elimu waliyopewa kuhusu Utawala Bora na Utunzaji wa Mazingira hivyo Watajitahidi kuzingatia maelekezo hayo kwa ajili ya Maendeleo ya Mtaa wa Isalavanu.
Vedasto Faustine Malima.
Afisa Habari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.