“Kila Mkuu wa Shule atakaye faulisha kwa alama ya ‘ A” atapata zawadi na Mwalimu wa somo husika aliyefaulisha na somo lake kupata A atapata zawadi kulingana na A zilizopatikana kwa somo lake” Hii itasaidia kuchagiza morali ya kazi kwa walimu hao.”
“ Tuhakikishe tunatunza nidhamu za wanafunzi mashuleni na Taaluma inapanda katika Shule zetu licha ya Serikali kuongeza majukumu ya kusimamia miradi ya maendeleo inayoletwa na kushushwa kwenye Shule zetu ya Miundombinu mbalimbali ya shule.
Bi Myovella ameendelea kuwapongeza Wakuu hao wa Shule za Sekondari 28 katika Halmadhauri ya Mji Mafinga kwa kusimamia vyema walimu waliochini yao ambao wameonyesha kutokuwa na malalamiko kwa Serikali hali iliyopelekea walimu hao kuendelea kulinda taswira ya walimu na Serikali ukizingati Mafinga ina walimu wengi lakini ina utulivu mkubwa.
Bi Myovella amewataka Wakuu hao wa Shule kuhakikisha wanatunza nidhamu ya walimu waliochini yao na wanafunzi wawapo mashuleni wasome wasitoroke.
Naye Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Mwalimu Stephen Shemdoe amesema katika kikao hicho Muungano wa Walimu wa Shule za Sekondari ( TAHOSSA) utafanya uchaguzi wa viongozi ngazi ya Halmashauri na kuzungumza kuhusu mafanikio na changamoto zinazowakabili.
Na Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.