MKURUGENZI HALMASHAURI YA MJI MAFINGA AIPONGEZA IDARA YA ELIMU MSINGI KWA USIMAMIZI MZURI WA MITIHANI YA DARASA LA SABA 2025 .
Wanafunzi wa Darasa la Saba katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga wamemaliza kufanya Mitihani yao ya Kumaliza Elimu ya Msingi iliyofanyika kuanzia tarehe 10 mpaka Tarehe 11 Mwezi huu wa 9 Mwaka 2025
.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Bi; Fidelica Myovella amesema anawapongeza Idara ya Elimu Msingi kwa Usimamizi Mzuri wa Mitihani ya Darasa la Saba kwa kuzingatia uwepo wa Amani na kutokuwepo na changamoto yoyote.
Naye Afisa Elimu Msingi Bi; Doroth Kobelo amesema kuwa idadi ya Wanafunzi Waliofanya Mitihani Jumla wapo 2905,Wavulana 1367 na Wasichana 1538.
“Idadi ya Shule za Wanafunzi Waliofanya Mitihani ya Darasa la Saba zilikuwa Jumla 44 kati ya hizo Shule za Serikali ni 31 na Shule binafsi ni 13." Amesema.
Pamoja na hayo Bi; Doroth ameshukuru Uongozi wa Halmashauri na Taasisi mbalimbali kwa kuhakikisha Mitihani kufanyika kwa Amani bila kuwepo na changamoto yoyote
.
Vedasto Malima.
Afisa Habari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.