Wapeni watoto Majina mazuri ya heshima, Mkiwapa majina mabaya yanaathiri sana ukuaji wao na baadae kusababisha kutokea ukatili kwa mtoto husika au kwa jamii inayomzunguka kutokana na jina alilonalo”
Kauli hiyo imetolewa na Ndugu, Martin Chuwa Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Iringa alipokuwa akitoa mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati ya kusimamia Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto( MTAKUWWA) ngazi ya Halmashauri ya Mji Mafinga.
Ndugu Chuwa ambaye ni Mwezeshaji amesema kuwa Majina mengi watoto wanayopewa hasa mabaya yanawafanya watoto hao wakikua kuishi maana ya majina yao au kutenda maovu wakipata uhalisia wa historia ya Majina yao, hivyo amewaomba wazazi kuhakikisha wanawapa watoto majina yenye heshima na si vinginevyo.
Akifungua Mafunzo hayo ya siku Moja Mkurugenzi Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema kuwa suala la ukatili halikubaliki popote na ndio maana Serikali inaweka Mikakati mathubutu ya kutokomeza ukatili ndani ya jamii kwa kushirikisha wadau, wananchi, taasisi za dini, asasi za kiraia na vyombo vya usalqma.
“ Ukatili Mkubwa wa Kijinsia unasababishwa na hali ya umaskini kwenye familia husika” hivyo lazima tuhakikishe ukatili unatokomwezwa kwa gharama yoyote” amesema Bi. Myovella
Lengo la mafunzo haya ya siku moja ni kuwakumbusha wajumbe majukumu yao na kuhakikisha Halmashauri ya Mji Mafinga kupitia Kamati hii ya MTAKUWWA inatoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya ukatili na kubuni mbinu za kuzuia ukatili wa kijinsia ndani ya jamii kwa kushirikisha wananchi.
Kamati ya MTAKUWWA awamu ya Pili inaundwa na wajumbe kutoka Dawati, Taasisi za Dini, Wazee, Makundi ya wanawake, Mahakama, Maafisa Ustawi wa Jamii, Menejimenti ya Halmashauri, wawakilishi wa wanafunzi wa Msingi na Sekondari pamoja na Afya.
Imeandaliwa na
Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu - Mji Mafinga
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.