MAFINGA TC YANG’ARA SHIMISEMITA 2025 TANGA, YANYAKUA VIKOMBE VITATU NA MEDALI
Posted on: August 29th, 2025
Halmashauri ya Mji Mafinga imehitimisha kwa kishindo Mashindano ya Shirikisho la Michezo kwa Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) 2025 jijini Tanga, kwa kunyakua vikombe vitatu na medali moja, ishara ya mafanikio makubwa katika Michezo.
Katika mashindano haya yanayomalizika leo tarehe 29 Agosti 2025, Mafinga TC imetwaa:
Nafasi ya pili katika mashindano ya Kwaya na Ngoma,
Nafasi ya tatu katika Uchoraji,
Na medali ya shaba (mshindi wa tatu) katika mbio za mita 1500 wanaume.
Akizungumza baada ya mashindano kumalizika, kiongozi wa timu ya Mafinga TC, Ndugu Mawasiliano Deule, amesema kuwa ushindi huo umetokana na ushirikiano madhubuti, juhudi na nidhamu ya hali ya juu miongoni mwa wanamichezo wote tangu maandalizi hadi siku za mashindano.
Aidha, ametoa shukrani kwa Uongozi wa Halmashauri ya Mji Mafinga ukiongozwa na Mkurugenzi Bi, Fidelica Myovella kwa ushirikiano walioupata wakati wote wa maandalizi na mashindano.
Mashindano ya SHIMISEMITA yamehitimishwa leo yakiwa yamebeba kauli mbiu “ Jitokeze kupiga kura kwa Maendeleo ya Michezo”.