Halmashauri ya Mji Mafinga imefanya Kongamano la kuwajengea uwezo na kuwakumbusha majukumu ya msingi Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa ambao wamechaguliwa hivi karibuni, katika kongamano hilo limehudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mufindi ikiwa ni katika sherehe za kuazimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika ambapo kauli mbiu ni “ Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo Yetu”.
Katika kongamono hilo ambalo mgeni rasmi ni Afisa Tawala Ndugu Robert Kilewo ambapo ameambatana na watoa mada mbalimbali kutoka vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Polisi, Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Jeshi la Uhamiaji ambao wote wametoa mada za kuwajengea uwezo na uadilifu pamoja na uwajibikaji katika maeneo yao ya kazi .
Washiriki katika kongamano hili wamekumbushwa kusimamia maadili na miongozo ya kazi zao ikiwemo kushiriki vikao vya maendeleo katika maeneo yao na pia kuibua miradi ambayo inapewa kipaumbele na wananchi ili kuhakikisha maendeleo yanafika kwa wakati pia wamesisitizwa kuwa na utaratibu wa kusoma mapato na matumizi ya Mitaa na Vijiji ili kuwajengea imani wananchi ambao wanawaongoza.
Aidha Watendaji na Wenyeviti ambao wameshirikia kongamao hilo wametakiwa kuhakikisha wanapinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na makundi mbalimbali katika jamii na pia kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo jeshi la polisi kuhakikisha wanatoa taaarifa kwa za vitendo vya ukatili ili kuweza kujenga jamii iliyo bora .
Katika kongamao hilo washiriki wamesisitizwa kuwa waadilifu na kuachana na vitendo vya rushwa kwani vimekuwa ni adui wa maendelo katika jamii na kusbabisha migogoro ambayo inapelekea uvunjifu wa amani pia wameaswa kutumia vitendea kazi vyo vizuri ikiwemo mihuri pamoja na matumizi bora ya ofisi ili kuhakikisha wanaleta maendeleo katika maneo yao.
Sambamba na nasaha hizo ambazo zimetolewa katika kongamano hilo la kuazimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika Watendaji wa Vijiji na Kata pia wametakiwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za Ulinzi na Usalama wa maeneo yao ikiwemo kutambua wageni katika maeneo yao na kusimamia uwandikishwaji wa watoto shuleni kwa darasa la kwanza na awali kwa mwezi ujao ili kuhakikisha jamii inaelimika na kupata elimu.
Pia mgeni rasmi Afisa Tawala wa Wilaya ya Mufindi ndugu Robert Kilewo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Dkt Linda Selekwa amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo ikiwemo fedha zinazo tolewa za miradi ya maendeleo na pia amipongeza Halmashauri ya Mji Mafinga kwa kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano jambo linalopelekea miradi kusongo mbele na wananchi kupata huduma.
Michael Ngowi
Afisa Habari Halmashauri ya Mji Mafinga.
Wajumbe mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wakifatilia Kongamano la miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika ambalo limetumika kuwajengea uwezo Watendaji na Wajumbe wa Serikali za Mitaa ambao wamechaguliwa hivi karibuni juu ya uwajibikaji na uadilifu katika kazi zao.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.