VIONGOZI WAPYA WA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA WAAPISHWA RASMI KWA AJILI YA KUANZA MAJUKUMU YAO
“Msingi Bora wa uongozi unaanzia ngazi za chini ni jukumu lenu ninyi viongozi wa serikali za mitaa ni kudumiasha amani katika mitaa yenu na kuleta maendeleo kwa wananchi kwa kushirikiana na Viongozi wa ngazi ya juu”
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga katika zoezi la kuwaapisha viongozi wapya wa serikali za mitaa wa kata ya Sao Hill na Bumilayinga katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Sao Hill.
Nae Mawasiliano Deule Afisa Utumishi Halmashauri ya Mji Mafinga amewataka viongozi wapya kufuata sheria za serikali na sio kuzipuuza kwani sheria ni kwaajili ya wananchi wote
“ Nendeni mkawe mfano wa kuigwa na jamii zenu msitumie uongozi kama fimbo ya kuwadhurumu watu, hakikisheni mnatenda haki kwa kufuata muongozo wa majukumu niliowasomea hapa na mwisho niwatakie kazi njema”. Amesema Deule
Uapisho huo umefanyika chini ya usimamizi wa Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Mafinga Gasper Kalinga pamoja na Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mufindi Bi.Sekela Kyungu.
Na: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.