Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Fedelica Myovela ameshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya stendi ya Matanana pamoja na Hospitali ya Mji Mafinga ikiwa ni kuazimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika yenye kauli mbiu “ Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo Yetu”.
Katika zoezi hilo la kufanya usafi limehudhuruwa na watumishi mbalimbali wa Halmashauri na wananchi wa Mafinga, na makundi mbalimbali ambapo Mkurugenzi Bi Myovella amewataka wananchi wa mji wa mafinga kuhakikisha wanafanya usafi katika maeneo yao ya biashara ili kuhakikisha ya nakuwa masafi wakati wote hii itasaidia kuepukana na magonjwa ya mlipoko katika maeneo yetu ya biashara .
Aidha ametoa rai kwa Watendaji na Wenyeviti wa Mitaa kuhakikisha wanakuwa na desturi za kupita katika masoko na kwenye maduka ili kuhamasisha zoezi la usafi liendelee kufanyika kila siku na kuacha kufanya usafi kwa mazoa ya kusubiri mwisho wa mwezi .
Pia Bi Myovella amewapongeza watumishi wote, wananchi na makundi mbalimbali ambayo yamejitokeza katika kufanya usafi na kuwasisitaza umuhimu wa kutunza mazingira na kufanya usafi katika maeneo yao na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha maeneo yanakuwa safi na salama pia Bi muyovella amepanda miti katika Hospitali ya Mji Mafinga ili kuhamasisha jamii kupanda miti katika maeneo yao.
Habari na Michael Ngowi
Afisa Habari Halmashauri ya Mafinga Mji
Picha mbalimbali katika zoezi la ufanyaji usafi Halmashauri ya Mji Mafinga ikiwa ni kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika .
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.