BENKI ya CRDB Tawi la Mafinga kupitia Mpango wa Keti-Jifunze imekabidhi madawati 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa ikiwa ni kuunga Mkono Jitihada za Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha wanafunzi wote Nchini wanapata Elimu Bora na katika Mazingira rafiki na salama.
Akipokea Madawati hayo mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa alisema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kujenga Miundombinu ya Madarasa na kuweka madawati na vifaa vya kujifunzia na Wadau wanafanya kuunga juhudi za Serikali kwa kiasi kikubwa lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kusomea.
“Wanafunzi Serikali imefanya nafasi yake, Wadau Hawa wa CRDB wamefanya nafasi yao na wamekuwa ni wadau wazuri wa Maendeleo katika Wilaya ya Mufindi sasa jukumu lililobaki ni ni lenu wanafunzi kusoma kwa bidii na kufaulu ili mtimize ndoto zenu”
Kwa uapande wake Meneja wa CRDB Kanda ya kati Chabu Mishwaro alisema Mpango huo wa keti-Jifunze unaotekelelezwa na Benki hiyo, unatekelezwa na nchi nzima ambapo lengo ni Kuunga Juhudi za Serikali kuhakikisha kila mwananfunzi anapata fursa ya kujifunza vizuri akiwa amekaa na siyo kurundikana katika dawati moja.
"Lengo la kutoa Madawati ni kuinua kiwango cha elimu katika shule zetu zote Nchi mzima ili kuongeza ufahuru kwa wanafunzi kutoka na na kujifunza katika mazingira rafiki na wezeshi.hakikisha tunapunguza msongamano wa wanafunzi kukaa kukaa katika dawati moja" Alisema.
Naye Mkurugenzi wa Mji Mafinga Fidelica Myovella alisema Dawati hizo zitapunguza Changamoto ya upungufu wa madawati 100 ambayo inaikabili shule hiyo.
"Tunawashukuru sana Benki ya CRDB kwa kuunga mkono Jitihada za Serikali za kuhakikisha wanafunzi wanapata Elimu katika mazingira Tulivu. Niwahakikishie tutayatunza madawati haya ili yaendelee kuleta manufaa kwa wanafunzi wetu”Alisema.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.